Diamond ‘Fine’, Nandy ‘Siwezi’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania

[Picha: K24TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mtandao wa YouTube ni moja ya mitandao ambayo wasanii wengi sana hupendelea kuweka kazi zao za muziki. Kama wewe ni shabiki na una kiu ya kutaka kujua ni ngoma gani imefanya vizuri zaidi YouTube kwa nchini Tanzania,  basi umefika sehemu sahihi. Zifuatazo ni ngoma tano ambazo zinatamba na kufanya vizuri sana nchini Tanzania kwa wiki hii kwenye mtandao wa YouTube:

Pakua Nyimbo za Ali Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Fine - Diamond Platnumz

Fine ni video ya kwanza kabisa kutoka kwenye EP ya First Of All ya kwake Diamond Platnumz. Utayarishaji wa video ya ‘Fine’ imeongozwa na TG Omori kutoka huko nchini Nigeria. ‘Fine’ ni video ambayo imeundwa na stori nzuri, uhalisia pamoja na ubora wa picha wenye viwango vya kimataifa. Bila shaka hii ni video ambayo ina hadhi ya kuchezwa kwenye kituo chochote cha runinga duniani. Aidha video hii iliweka rekodi nyingine kwenye muziki wa Bongo baada ya kutazamwa mara Milioni 1 ndani ya saa 15 tu, kitu ambacho ni nadra sana kutokea kwenye Bongo Fleva.

https://www.youtube.com/watch?v=QOGi0Qp_ciA

Nawaza - Diamond Platnumz

Ngoma ya Nawaza imezidi kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na ujumbe mzito ambao Diamond alikuwa anafikisha kupitia ngoma hiyo. Kwa mujibu wa Diamond Platnumz, alitanabaisha kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni kuwa hii ni mojawapo ya ngoma zake pendwa kwenye EP yake ya First Of All.

https://www.youtube.com/watch?v=njxSViOtBbY

Mtasubiri - Diamond Platnumz ft Zuchu

Kama haujasikia ‘Mtasubiri’ kwenye redio basi bila shaka utakuwa umesikia na kuuona kwenye mitandao ya kijamii. Huu ni wimbo ambao Diamond Platnumz na Zuchu wanasifiana kwa kupeana mapenzi mazito huku wakitupa vijembe kwa watu wasiopenda penzi lao kuwa waache kuwafatilia kwani mapenzi yao hayawahusu. Mtasubiri ni ngoma ya tatu kwa Diamond Platnumz kushirikiana na Zuchu baada ya wawili hao kufanya ‘Cheche’ na ‘Litawachoma’.

https://www.youtube.com/watch?v=2WnDQnJ4UDY

Siwezi - Nandy

Baada ya ukimya wa takriban miezi mitatu, hatimaye Nandy amerudi tena na

ngoma yake mpya ya kuitwa Siwezi ambayo imepokelewa kwa dhati na mashabiki zake. Siwezi ni ngoma ambayo Nandy analilia mapenzi. Nandy anaweka wazi maumivu anayoyapitia baada ya kutendwa na mwanaume aliyempenda sana. Ndani ya siku moja tu tangu kuachiwa kwake, Siwezi imekuwa ngoma kubwa sana kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara laki saba arobaini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=FuK_yKDdmHo

Bakhresa - Harmonize

Kama kuna kitu ambacho Harmonize anavutiwa nacho ni kuona mtu mwenye uwezo kiuchumi anasaidia watu bila kujigamba, kujiona au kujikweza na ndio maana aliamua kutoa Bakhresa ngoma ambayo anamsifia Said Salim Bakhresa ambaye ni tajiri kutoka Tanzania asiyependa kabisa makuuu. Kufikia sasa audio ya ngoma hii imetazamwa mara Milioni moja nukta nane kwenye mtandao ikiwa na siku kumi na tatu tu tangu kuachiwa kwake.

https://www.youtube.com/watch?v=OtORnRuDJ-g

Leave your comment