Wasanii 5 wa Bongo Waliozua Gumzo Baada ya Kukosa Uteuzi Kwenye 2022 Tanzania Music Awards

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Ali Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Habari kubwa nchini Tanzania kwa sasa ni kuhusu tuzo za muziki ambazo siku chache zilizopita BASATA walitangaza majina ya wasanii ambao wamepata uteuzi kwenye tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika April Mosi mwaka huu.

Ali Kiba anaongoza kwa kupata teuzi nyingi baada ya kuonekana kwenye vipengele 8 akifuatiwa na rapa Professor Jay aliyetajwa mara 7 huku Nandy na Harmonize walikwa wametajwa kwenye vipengele 6.

Pakua Nyimbo za Vanessa Mdee Bila Malipo Kwenye Mdundo

Baada ya BASATA kuachia majina ya wasanii ambao wameteuliwa kuwania tuzo, wasanii na wadau wengi wa muziki ikiwemo Baba Levo, Wakazi na Damian Music wameonekana kusikitishwa na baadhi ya vipengele kwenye tuzo hizo.

Wafuatao ni wasanii watano kutoka Tanzania ambao walizua mjadala baada ya majina yao kukosekana kwenye tuzo hizo:

 Wasanii wa Wasafi

Wasanii wote wa Wasafi kuanzia Diamond Platnumz, Rayvanny, Mbosso, Lavalava, Zuchu na Queen Darleen majina yao hayakuwepo kwenye orodha ya wasanii wanaotarajiwa kuwania tuzo hizo, kitu ambacho kilizua mjadala mkubwa sana mtandaoni. Baraza la Sanaa La Taifa ilitoa muongozo kupitia barua kwa kueleza kuwa Wasafi hawakuleta kazi zao za kimuziki kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya kuingia kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo na ndio maana hakuna msanii hata mmoja wa kwenye lebo hiyo ametajwa kuwania tuzo.

Soma Pia: Ommy Dimpoz ‘Umeniweza’ na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

Jay Melody

Ni ukweli ulio wazi kuwa Jay Melody alifanya kazi kubwa sana kwa mwaka 2021 kwani aliweza kutoa ngoma mbalimbali kama Huba Hulu, Sambaloketo, Najieka na nyinginezo ambazo ziliburudisha mashabiki . Ingawaje, jina lake halikutokea kwenye orodha ya wasanii wanaowania tuzo. Jay Melody aliweka wazi kuwa uongozi wake ulifuata kila utaratibu ikiwemo kupeleka baadhi ya ngoma zake BASATA ili kuwania tuzo hizo .

Ibraah

Nyota huyu wa Konde Gang alifanya kazi kubwa sana mwaka 2021 kwa kuachia EP yake ya Karata Tatu pamoja na ngoma yake ya Jipinde ambayo ilifanya vizuri sana. Pamoja na kufanya maajabu 2021, Ibraah hajapata uteuzi wowote kwenye tuzo hizo za muziki. Harmonize pamoja na Anjella ndio  wasanii pekee kutokea Konde Gang kutajwa kwenye tuzo hizo.

Mac Voice

Wengi walitegemea Mac Voice kutokea Next Level Music angekuwepo kwenye tuzo hizo hasa kipengele cha msanii Bora chipukizi lakini haikuwa hivyo kwani msanii huyo ambaye alitikisa Tanzania baada ya kuachia EP yake ya My Voice Oktoba 2021 hakuonekana kwenye tuzo. Kufikia sasa bado haijafahamika sababu hasa za Mac Voice kukosekana kwenye tuzo huku wengi wakishuku kuwa huenda fundi huyo hakupeleka kazi zake kama ambavyo bosi wake Rayvanny hakuwasilisha kazi zake kwa ajili ya kuwania tuzo hizo.

Hanstone

Ukweli ni kwamba Hanstone aliupiga mwingi sana kwa mwaka 2021 kwa kuachia EP yake ya kuitwa ‘Amaizing’ ambayo ilisikika kila sehemu hapa nchini Tanzania. Hanstone ambaye alikuwa ni msanii wa WCB wengi walishuku kuwa huenda angeonekana kwenye kipengele cha msanii bora chipukizi kutokana na ngoma zake kusikika sana hakuonekana kwenye kipengele chochote za tuzo hizo . 

Leave your comment