Ommy Dimpoz ‘Umeniweza’ na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Vanessa Mdee Bila Malipo Kwenye Mdundo

Katika harakati za kuhakikisha kuwa wanaburudisha mashabiki wao wasanii wa Tanzania wamezidi kuachia ngoma ambazo bila shaka zimeweza kufanya tasnia ya muziki nchini kuchangamka. Zifuatazo ni ngoma mpya ambazo zimeachiwa na wasanii wa Tanzania kwa wiki hii:

On My Way - Manengo ft Nay Wa Mitego & Moni Centrozone

Huu ni wimbo ambao wasanii hawa wa Hiphop wanazungumzia mambo mbalimbali ya kimaisha kama mahusiano, pesa, kujikweza na mambo mengineo. Tangu kuachiwa kwake , imekuwa ni ngoma pendwa kwa wapenda muziki wa rap Tanzania nzima.

https://www.youtube.com/watch?v=-PNdTx6jz9g

Soma Pia: Diamond, Harmonize Watawala Nyimbo Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Umeniweza - Ommy Dimpoz 

Ommy Dimpoz amerudi na wiki hii gwiji huyu aliachia kibao chake kipya cha kuitwa ‘Umeniweza’ ambacho ndani yake haoni haya kueleza namna gani ambavyo amepagawa na penzi analopewa na mwenza wake, huku akimsifia na kummwagia pongezi za kutosha.

https://www.youtube.com/watch?v=AdyW4JvmmBA

Blaza - Young Dee ft Cheqbob

Huu ni wimbo ambao Young Dee amelenga kuzua taharuki kwani kupitia ngoma ameweza kutupa maneno ya kashfa kama Young Killer kuwa amepotea kimuziki lakini pia amewataja Young Lunya na Country Wizzy kuwa ni marafiki zake.

https://www.youtube.com/watch?v=pXtUPK0JRWI

Oh My - Young Killer ft Mzee Yusuph

Kwenye ngoma hii Young Killer anaeleza kwa undani jinsi ambavyo amezama kwenye penzi zito na mwandani wake. Young Killer anatumia uwezo wake wa kurap kumwambia mpenzi wake atakavyoumia siku penzi lao likienda na maji.

https://www.youtube.com/watch?v=4XDPdGSkcPE

Sinyorita Remix - Lony Music ft Dully Sykes

Baada ya kuachia Sinyorita wiki tatu zilizopita, wiki hii Lony Music ambaye anachipukia kwenye Bongo Fleva aliachia ‘Sinyorita Remix’ ngoma ambayo ndani yake amemshirikisha Dully Sykes. Mashahiri ya ngoma hiyo kwa ujumla ni ya kumsifia mwanamke.

https://www.youtube.com/watch?v=ni14JU1NR9I

Leave your comment