Diamond ‘Gidi’, Zuchu ‘Mwambieni’ na Ngoma Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii
4 March 2022
[Picha: YouTube]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Wiki ya kwanza kabisa ya mwezi Machi imewadia na bila shaka utakuwa na hamu ya kufahamu ni ngoma gani ambazo zinasikilizwa zaidi nchini Tanzania wiki hii kwenye mtandao wa YouTube. Makala hii imelenga kukupitisha kwenye ngoma tano ambazo zinafanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube kwa wiki hii:
Pakua Nyimbo za Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo
Gidi - Diamond Platnumz
Diamond Platnumz amezidi kuonesha ubabe wake kwenye mtandao wa YouTube kwani ngoma yake ‘Gidi’ imezidi kufanya vizuri kwenye mtandao huo. Kufikia sasa ‘Gidi’ imeshatazamwa mara Milioni 3.6 kwenye mtandao huo ikiwa ndio inayoongoza kufanya vizuri zaidi kwa wiki hii.
Soma Pia: Diamond ft Wizkid, Anjella ft Ibraah na Collabo Zingine Bongo Zinazosubiriwa Sana na Mashabiki
Yanga Tamu - Marioo
Wale wapenzi wote wa mpira hasa timu ya Yanga bila shaka wameweza kurahani ngoma hii ya ‘Yanga Tamu’ ambayo ni kama remix ya ‘Bia Tamu’ kutoka kwa Marioo. Ikiwa zimepita siku 11 tu tangu kuachiwa kwake, ngoma hii ishatazamwa mara laki saba ishirini na nane kwenye mtandao wa YouTube.
Omoyo Remix - Jane Miso & Harmonize
Ngoma ya ‘Omoyo Remix’ inazidi kuchanja mbuga kwenye mtandao wa YouTube. Hii pengine ni kutokana na mbinu nzuri za matangazo zilizotumika na Harmonize wakati anaachia ngoma pamoja na ubora wa kimashairi, mdundo na vionjo alivyotumia Harmonize na Jane Mix katika kibao hiki.
Pakua Nyimbo za Navy Kenzo Bila Malipo Kwenye Mdundo
Mwambieni - Zuchu
Kila shabiki wa muziki mzuri kutoka Tanzania tayari ameshasikiliza ngoma ya ‘Mwambieni’ pamoja na kuangalia video ya wimbo huo ambayo imejawa na uigizaji mzuri, uhalisia pamoja na vichekesho vitu ambavyo vimepelekea ngoma kubwa mno. Kufikia sasa, ‘Mwambieni’ imeshatazamwa mara Milioni 4.8 huko YouTube.
Toroka - Anjella ft Harmonize
Hii ni ngoma ambayo imemleta Anjella mpya ambaye anaonekana kufurahia maisha ya kustarehe na ‘kula bata’ hasa nyakati za usiku kwenye klabu na sehemu za starehe. Kufikia sasa, video ya ngoma hii imeshatazamwa mara Milioni 1.9 kwenye mtandao wa YouTube.
Leave your comment