Diamond ft Wizkid, Anjella ft Ibraah na Collabo Zingine Bongo Zinazosubiriwa Sana na Mashabiki

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Moja ya vitu ambavyo vinazidi kung'arisha kiwanda cha muziki nchini Tanzania ni hulka ya wasanii watanzania kupendelea kutoa ngoma na wasanii wengine wawe wa ndani au nje ya nchi. Mwaka 2021 wasanii kutoka Tanzania waliweza kuburudisha masikio ya wasikilizaji wao kwa kuachia ngoma za ushirikiano kama ‘Baikoko’, ‘Ndombolo’, ‘Iyo’, ‘Beer Tamu’ na ngoma nyingine nyingi ambazo wasanii watanzania waliamua kuunganisha nguvu na kutengeneza kitu kimoja.

Pakua nyimbo za Marioo Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwaka huu wa2022 mambo yanatarajiwa kuwa sukari zaidi kwenye eneo hilo la collabo kwani kuna viashiria kuwa himaya ya Bongo Fleva itapokea collabo nyingi hapo mbeleni. Zifuatazo ni collabo tano ambazo zinasubiriwa kwa mwaka 2022:

Rayvanny na Marioo

Pengine Rayvanny na Marioo waliona kuwa watanzania hawajatosheka na ‘Te Quiero’ na ndio maana wasanii hao siku chache zilizopita walionekana wakiwa studio wakirekodi ngoma ya pamoja. Hii inakuja baada ya Rayvanny kuchapisha video inayomuonesha akiwa na Marioo maeneo ya studio huku watayarishaji wa muziki kama Sound Boy pamoja na S2kizzy wakiwepo pia, hivyo kuashiria kuwa muda wowote mvua ya burudani kutoka kwa wasanii hawa inaweza kunyesha.

Diamond Platnumz na Wizkid

Kama wewe ni shabiki wa Diamond Platnumz huna budi kujifunga mkanda na kusubiri kwani Diamond na Wizkid tayari wana ngoma ya pamoja kwa ajili yako. S2kizzy ambaye aghalabu hushiriki kuandaa kazi za ‘A Boy From Tandale’ alithibitisha ujio wa collabo Agosti mwaka 2021 na kudokeza kuwa wasanii hao wamesharekodi  ngoma tatu za pamoja na ni suala la muda mpaka collabo hiyo iingie sokoni.

Jux na Bontle Smith

Kwa muda sasa, Jux amekuwa anafanya collabo na wasanii wa ndani ila hivi karibuni ameonesha kubadilisha njia baada ya kuonekana akiwa studio na mwanamuziki kutoka Africa kusini Bontle Smith. Kupitia akaunti ya Instagram, mtayarishaji wa muziki S2kizzy alidokeza kuhusu collabo hiyo baada ya kuchapisha video ikimuonesha akiwa anarekodi ngoma na fundi huyo wa Amapiano kutoka Afrika Kusini.

Diamond Platnumz na G Nako

Hii ni collabo ambayo inasubiriwa kwa muda mrefu sasa na mashabiki wa muziki ambao walifahamu kuhusu collabo hii baada ya Diamond Platnumz kuacha maoni kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa wimbo ambao amefanya na G Nako ni mkali sana. Collabo hii kama itatoka itazidi kukoleza utamaduni wa msanii Diamond Platnumz kufanya collabo na wasanii wa Hip-hop nchini Tanzania. Kufikia sasa ameshafanya collabo na wasanii kama Professor Jay pamoja Young Killer.

Ibraah na Anjella

Akiwa anajibu maswali ya mashabiki zake kupitia Instastory mwaka jana, Anjella alidokeza kuwa kufikia sasa ameshafanya ngoma takriban tatu na Ibraah ambaye pia anatokea Konde Gang na kuwa ni suala la muda tu mpaka ngoma hizo itoke.

Leave your comment