Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video ya ‘Mi Amor’

Picha: Marioo YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Marioo ametimiza ahadi aliyoiweka kwa mashabiki zake baada ya kuachia video ya ngoma yake ya ‘Mi Amor’ ambayo ameimba na mwanamuziki kutokea Kenya Jovial.

Pakua Nyimbo za Marioo Bila Malipo Kwenye Mdundo

Video ya ‘Mi Amor’ inaletwa kwa mashabiki zikiwa zimeshatimia takriban wiki tatu tangu audio ya ngoma hiyo ambayo imetayarishwa na Kimambo Beats iingie sokoni na kuweza kufanya vizuri.

Video ya ‘Mi Amor’ inahadithia stori ya wapenzi ambao wanapendana haswaa na wanatumia muda wao wa pamoja kujivinjari kwenye sehemu mbalimbali. Marioo anaoneka akila raha kati kati ya eneo zuri la shamba la minazi huku akimuimbia mpenzi huku Jovial akionekana akipata huba eneo la ufukweni.

Kama ambavyo Madee alimtumia Dogo Janja kama mhusika kwenye video yake "Sema", ubunifu wa Marioo kumtumia rapa na muigizaji Quick Rocca kama mhusika kwenye video hii ni kitu kingine ambacho bila shaka kimevutia macho ya watazamaji.

Video hii imetayarishwa na Director Folex ambaye kufikia sasa ameshafanya video tofauti tofauti kama ‘Kushki’ ya Chege na Saraphina, ‘Nitakucheki’ ya Rapcha pamoja na ‘Pekecha’ ya Saraphina.

‘Mi Amor’ ni video ya kwanza ya muziki kutoka kwa Marioo kwa mwaka 2022. Kufikia sasa, imeshatazamwa mara ishirini na sita elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=aU9Gmomi02Q

Leave your comment