Nyimbo Mpya: Harmonize ‘Omoyo’ Remix, Rayvanny ‘Flowers II’ EP na Ngoma Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwezi Februari unazidi kunogeshwa na wasanii tofauti tofauti kutokea Tanzania ambao wamekuwa wakitoa ngoma ili kukata kiu ya burudani za mashabiki zao. Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka kwa wasanii wa Tanzania zilizotoka wiki hii:

Pakua Nyimbo Zake Kusah Bila Malipo Kwenye Mdundo

Omoyo Remix - Harmonize & Jane Miso

Huu ni wimbo ambao Harmonize anaulaumu moyo wake kwa kumshawishi kufanya matendo mabaya. Ukweli ni kwamba ukiweka kando mashahiri yaliyojaa ucheshi na ujumbe, sauti nzuri ya Jane Miso kwenye kiitikio ni kitu kingine kilichopamba ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=Luj_vFdImVs

X - Kusah

‘X’ ni ujumbe wa Kusah kwa mpenzi wake wa zamani ambaye haishi kufuatilia mahusiano ya Kusah. Ngoma hii imeundwa na mashahiri chokozi na ya kuudhi ambayo yatamuingia yeyote ambaye hapendi mahusiano yako yawe mazuri.

https://www.youtube.com/watch?v=5cDFuIPkFrY

Flowers II EP – Rayvanny

EP hii ni zawadi ya Rayvanny kwa mashabiki zake haswaa katika msimu huu wa Valentine Ngoma zilizopo kwenye EP hio kama ‘Te Quiero’ na ‘I Miss You zina maudhui ya mapenzi. 

https://www.youtube.com/watch?v=0PD7VbRnTCU

Daktari wa Mapenzi EP - Bonge La Nyau

Rapa Bonge La Nyau wiki hii aliamua kuvunja ukimya wake wa muda mrefu baada ya kuachia EP yake ya ‘Daktari wa Mapenzi’. Mashabiki wengi wameonekana kuipenda kutokana na ngoma zilizopo kweye EP hiyo kuwa na mashahiri mepesi ambayo yanaimbika kwa urahisi.

https://www.youtube.com/watch?v=IvFxEfWNSeQ

Sitamani - RJ The Dj ft Lody Music & Young Lunya

Hii ni ngoma ambayo Lody Music na Young Lunya wanashirikiana kuonesha namna ambavyo wamezama kwenye penzi zito kiasi cha kutotamani tena kuwa na mtu mwingine kwenye mahusiano.

https://www.youtube.com/watch?v=LX2CLMjCduk

Leave your comment