Nyimbo Mpya: Bonge La Nyau Aachia EP Yake ‘Daktari Wa Mapenzi’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Bonge La Nyau ameachia EP yake mpya kabisa ya kuitwa ‘Daktari Wa Mapenzi’.

Kama jina linavyoashiria, ‘Daktari wa Mapenzi’ ni EP ambayo imesheheni jumla ya ngoma sita za moto ambazo zote zinagusia suala zima la mapenzi; kitu ambacho wengi wametafsiri kuwa ni katika kuadhimisha msimu huu wa Valentine.

Pakua Nyimbo za Kayumba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Wasanii walioshirikishwa kwenye EP hii ni pamoja na Kayumba kwenye ‘Umenikosea’, Dayo ndani ya ‘Dam Dam’, Silvana kwenye ‘Nimechoka’ pamoja na Born Eyes kwenye ‘Waridi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Flowers II’ EP

Kikubwa kuhusu mradi huu ni kuwa Bonge la Nyau pamoj na ukubwa wake ameweza kufanya kazi na watayarishaji wa muziki wanaochipukia kama vile Dady Final, Bengs pamoja na Swabri Made It ambaye amehusika kutayarisha ‘Ndombolo’ ya kwao Kings' Music ambayo ni lebo ya Ali Kiba.

EP hii ni mradi wa kwanza wa Bonge La Nyau kwa mwaka huu wa 2022. EP hio inakuja baada ya miezi sita ya ukimya kutoka kwa msanii huyo ambaye mara yake ya mwisho kuachia ngoma ilikuwa ni Julai mwaka 2020 alipoachia  ‘Madharau Part 1’ iliyofanya vizuri nchini.

Leave your comment