Nyimbo Mpya: Maua Sama Aachia Ngoma Mpya ‘Shukurani’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri kutokea nchini Tanzania Maua Sama amezifuta kupeperusha vyema bendera ya muziki nchini Tanzania baada ya kuachia ngoma yake mpya kabisa aliyoipa jina la "Shukurani".

‘Shukurani’ ni ngoma yenye vionjo vya RnB na Bongo Fleva na huu ni wimbo makhususi kabisa ambao Maua anamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea.

Pakua Nyimbo za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kupitia kibao hiki, anakiri kabisa kuwa pamoja na kwamba kuna watu ambao siku zote wamekuwa wakitaka kumrudisha nyuma , mara zote Mwenyezi Mungu amekuwa akimpigania.

"Milango inazidi funguka na bado I am winning. Nikitazama nilipotoka i am grateful umenibariki. Wanadhani taa yangu itazima na bado watasubiri sana. God's making me shine like a star kila nnachomuomba ye hufanya," anaimba Maua Sama kwenye aya ya pili ya ngoma hii.

Ngoma hii bila shaka imemleta Maua Sama mpya kwani maudhui ya ngoma hii ni ya tofauti kwani yamelenga katika kutoa shukran kwa Mwenyezi Mungu kitu ambacho pia Tommy Flavour alishawahi kufanya kwenye ‘Jaja’, Ommy Dimpoz pia alifanya kwenye ngoma ya ‘Ni Wewe’ na hata Nandy pia alifanya ngoma ya kutoa shukran kwenye ‘Wanibariki’.

‘Shukurani’ imetayarishwa na Jaythan Mirra huku maandalizi ya mwisho ya ngoma hii yakishughulikwa na Hermy B kutoka B Hitz ambaye ameshafanya kazi na wasanii kama Vanessa Mdee pamoja na AY.

https://youtu.be/5SUefw-MUls

Leave your comment