Darassa Amtambulisha Msanii wa Kwanza Kwenye Lebo Yake ya CMG

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa mashuhuri kutokea Tanzania Darassa CMG amemtambulisha msanii wa kwanza kwenye lebo yake ya Classic Music Group anayeitwa Sani Boy.

Akiwa kwenye onesho la kimuziki eneo la Kidimbwi Beach, Darassa alisindikizwa na wasanii kama Jux, Marioo na Ben Pol. Kipindi akiwa kwenye onesho hilo, alimtambulisha msanii huyo.

Soma Pia: Nandy Atangaza Ujio wa Colabo Zake na Davido, Patoranking, Sauti Sol na Dula Makabila

Darassa alimtambulisha msanii huyo ambaye pia amekuja na EP yake ambayo ameipa jina la ‘Anaitwa Sani Boy’. EP hio imesheheni ngoma tano ambazo ni ‘Ridhiki Yangu’, ‘Anakuzuga’, ‘New Generation’, ‘Tuishie Hapa’ pamoja na ‘Pomp Pomp’ ambayo amemshirikisha Darassa.

Aidha, pamoja na kwamba Sani Boy ni msanii mchanga lakini EP yake imetayarishwa na watayarishaji wakubwa wa muziki kutoka Tanzania kama Kapipo na SBO huku maandalizi ya mwisho yakiwa yameshughulikiwa na Mr Touch.

Soma Pia: Rayvanny Atangaza Ujio wa EP ya ‘Flowers II’

Sani Boy ameingia kwenye orodha ya wasanii ambao wametambulishwa na kuachia EP hapo hapo, wasanii wengine ambao walitambulishwa na kuachia EP kutoka Tanzania ni pamoja na Mac Voice kutoka Next Level Music, Zuchu kutoka WCB pamoja na Ibraah kutokea Konde Gang.

Leave your comment