Nyimbo Mpya: Country Wizzy Aachia Ngoma Mpya ‘Speed’ [Video]
31 January 2022
[Picha: YouTube]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Rapa mkali kutokea nchini Tanzania Country Wizzy ameachia ngoma mpya ya ‘Speed’ wiki kadhaa baada ya kutoka lebo ya Konde Music Worldwide.
‘Speed’ ni ngoma ya Hip-hop ambayo Country Wizzy anaonesha uwezo wake wa kuchana mistari. Kwenye mashairi ya ngoma hii, Country anagusia namna ambavyo anakubalika na rafiki zake wa mitaani huku akituma salamu kwa watu wasiompenda kuwa hayuko kama zamani kwani sasa hivi yuko ‘Speedy’.
Soma Pia: Diamond, Rayvanny Watajwa Miongoni Mwa Wasanii Wa Afrika Waliotazamwa Zaidi YouTube 2021
"Utanikuta na gang machawa sitoki nao, haters faking mi sishoboki nao na hata wakitaka tuondoke mi siondoki nao. 24/7 niko high niko sticky sticky maswali mengi kuwa why nje siskiki wanasema mi malaya eti nacheat cheat. Dada zao wanalia mi ni player huku manigga mikono in the air," anaimba Country kwenye aya ya kwanza.
Ngoma hii imetayarishwa na S2kizzy ambaye ni mojawapo ya watayarishaji wakubwa wa muziki nchini Tanzania. Kufikia sasa, ameshafanya kazi na wasanii wengi wakubwa kutoka Tanzania kama Diamond Platnumz, Rayvanny, Whozu, Vanessa Mdee na wengineo huku maandalizi ya ngoma yakishughulikwa na The Mix Killer.
Soma Pia: Aslay Adokeza Ujio wa Wimbo Mpya Baada ya Kimya Kirefu
‘Speed’ ni ngoma ya kwanza kutoka Country Wizzy tangu atoke Konde Gang na pamoja na kwamba bado rapa huyo hajatangaza rasmi atajiunga na lebo gani ya muziki, wengi wanashuku kuwa huenda akarudi kwenye lebo yake ya zamani ya Rooftop Entertainment au akaanzisha lebo yake mwenyewe na kuanza kusimamia wasanii.
Leave your comment