Aslay Adokeza Ujio wa Wimbo Mpya Baada ya Kimya Kirefu

[Picha: Aslay Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki wa bongo Aslay ambaye pia ni mwanachama wa zamani wa bendi la Yamoto amedokeza ujio mpya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu mno.

Ukimya wa Aslay kwenye muziki umeibua maswali mengi huku baadhi ya mashabiki wake wakitaka arudi kwenye muziki na kung'aisha nyota yake.

Soma Pia: Mkubwa Fella Azungumzia Tetesi za Uhasama Kati ya Mbosso na Aslay

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aslay alichapisha video iliyomwonyesha akiusikiliza wimbo ambao unatarajiwa kutoka hivi karibuni. Kama kawaida ya Aslay, ngoma hii mpya imeandikwa kiushairi na inahusu maumivu anayopitia kwenye mapenzi.

Sauti yake nyororo inasikika ikiimba kwa hisia nzito mno kwenye ngoma hiyo. Japo Aslay hakutoa maelezo yoyote, mashabiki wengi walionyesha furaha na ujio huu mpya.

Soma Pia: Aslay vs Marioo: Nani Bora Zaidi katika mziki wa RnB?

Wengi, vile vile, walipendezwa na ngoma hiyo ya Aslay na kuonyesha hamu kubwa ya kuisikiliza.

Aslay hakufichua tarehe kamili ambayo ngoma hiyo itaachiwa, wala alipofikia na utengenezaji wake. Kando na wimbo wa ‘Mama’ alioutoa takriban miezi minne iliyopita, Aslay hajatoa kazi yake binafsi kwa takriban mwaka mmoja sasa.

Video ya mwisho aliyoachia ilikuwa ya wimbo wa ‘Nashangaa’ mnamo tarehe 16, mwezi Januari mwaka jana. Aslay, hata hivyo, kwa siku za hivi karibuni ameshirikishwa na wasanii wengine kwenye kazi zao. Aslay ni mmoja kati ya wasanii wa bongo ambao wamekuwa kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania kwa muda mrefu sana.

Leave your comment