Mkubwa Fella Azungumzia Tetesi za Uhasama Kati ya Mbosso na Aslay

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Aliyekuwa meneja wa kundi la Yamoto Band Mkubwa Fella amezungumza kwa undani kuhusu tetesi zilizosambaa kwa muda mrefu kuwa Mbosso na Aslay hawana maelewano mazuri.

Akiongea kwenye kipindi cha The Switch, Mkubwa Fella ambaye ni kama mlezi wa wasanii hao alisema kuwa kwa upande wake haoni kama kuna mgogoro wowote baina ya wasanii hao.

Soma Pia: Aslay vs Marioo: Nani Bora Zaidi katika mziki wa RnB?

Kwa mujibu wa Mkubwa Fella, mashabiki ndio huwashindanisha wasanii hao wawili.

"Ukiona hivyo kuna mashabiki tu wanaingia tu kwenye midomo midomo lakini mi naamini wale wote ni ndugu na wamezaliwa kwenye koo moja. Kwa sababu mwisho wa siku sasa hivi Mbosso ana management yake alafu ukiangalia na Aslay ana management yake lakini mwisho wa siku wao wafanye kazi mambo yaende," alizungumza Mkubwa Fella.

Soma Pia: Mkubwa Fella Azungumzia Kuvunjika kwa Yamoto Band, Ukimya wa Aslay

Mkubwa Fella ambaye pia ni mmojawapo ya wasimamizi wa kimuziki wa mwanamuziki Diamond Platnumz aliwahasa wasanii hao yaani Aslay pamoja na Mbosso waendelee kufanya kazi na ikibidi watoe ngoma ya pamoja.

"Kuna siku wakae na wenyewe waangalie wafanye kitu kimoja kwa pamoja ukiangalia Beka yuko smart ukiangalia na Enock yuko smart wao nao wawe masmart wawili wafanye kitu cha pamoja inatosha," alimalizia Mkubwa Fella.

Kundi la Yamoto lilikuwa maarufu sana nchini Tanzania kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 ambapo lilivunjika.

Leave your comment