Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video Mpya ‘Utu’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri kutokea nchini Tanzania na bosi kutokea lebo ya King's Music Alikiba ameachia video ya ngoma yake ‘Utu’.

‘Utu’ ni ngoma namba 14 kwenye albamu ya Alikiba ambayo inaitwa ‘Only One King’, albamu ambayo ilitoka mwezi Oktoba mwaka 2021.

Soma Pia: Harmonize Amtaka Alikiba Kuburudisha Siku ya Kumposa Mpenzi Wake

Kutokana na mashahiri yake kuweza kuimbika nakukaririka kwa urahisi, ngoma ya ‘Utu’ imekuwa ni mojawapo kati ya nyimbo bora kwenye albamu.

Stori ya video ya ‘Utu’ imeendana na mashairi ya wimbo kwani ndani yake inamuonesha Alikiba akiwa na binti mrembo maeneo ya milimani yaliyojawa na utulivu. Akiwa na binti huyo, Kiba anamwimbia na kumsifia jinsi alivyo na tabia njema pamoja na ‘Utu’.

Kilichovutia zaidi kwenye video hii ni mandhari yaliyotumika ambayo ni Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu zaidi barani Afrika. Aidha, hii ni video ambayo unaweza kutazama na mtu yeyote bila kujali umri.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Tarehe ya Tamasha la Afro East Carnival

Pamoja na kwamba wimbo ni wa mapenzi, maadili na hata mavazi ambayo wamevaa Alikiba na Nana Dollz pia hayana utata. Director Ivan ambaye ni moja kati ya watayarishaji bora wa video kutoka nchini Tanzania ndiye aliyetayarisha video hii.

Aidha, Ivan pia alihusika kutayarisha video ya ‘Teacher’ ya kwake Harmonize pamoja ‘Unachezaje’ ya Diamond Platnumz.

‘Utu’ ni video ya saba kutoka kwa kwenye albamu ya ‘Only One King’. Kutoka kwenye albamu hiyo, video nyingine ambazo zishatoka ni pamoja na ‘Infedele’, ‘Oya Oya’, ‘Bwana Mdogo’ aliyomshirikisha Patoranking, ‘Salute’ aliyomshirikisha Rude Boy na nyinginezo mingi.

https://www.youtube.com/watch?v=PkXxm2tCtgs

Leave your comment