Harmonize Atangaza Tarehe ya Tamasha la Afro East Carnival

[Picha: Tuko]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza tarehe kamili ambayo tamasha lake la Afro East Carnival litafanyika. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alidhibitisha kuwa tamasha hilo litafanyika tarehe tano mwezi wa tatu.

Aliongezea kuwa tiketi za kuhudhuria tamasha hilo zitaingia sokoni mnamo tarehe kumi mwezi wa pili. Harmonize alisisitiza kuwa tamasha hilo litakuwa moja wapo ya hafla kubwa zaidi kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania kwa mwaka huu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Ngoma Mpya ‘Mwaka Wangu’

Alifichua kuwa wasanii wakubwa Afrika Mashariki watatumbuiza kwenye tamasha hilo. Alionyesha hamu kubwa ya kujumuika kwenye jukwaa pamoja na mastaa mbali mbali.

Harmonize, hata hivyo, alisema kuwa atatangaza ukumbi wa hafla hiyo pamoja na ada ya kiingilio.

"This one going 2b the biggest news all East African top artist in one stage I can't wait to share the biggest stage with my brother's & sister's 5/3/2022/ in Dar es Salaam Big line up all East African super stars tickets out 10/2/2022/ utakapo sikia zikishatoka hiiii sio yakusikilizia ...!!!! I will be back with (venue) nitaawambia uwanja gani & kiingilio shingapi ..!!!! Let's go 5/3/2022," chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu ‘Mwambieni’, Harmonize ‘Mwaka Wangu’ na Ngoma Zingine Mpya Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Mwishoni mwaka jana, Harmonize alidokeza ujio wa tamasha hili. Wakati huo alisema kuwa anapanga kufanya tamasha mapema mwaka huu, na yaonekana Harmonize ametii ahadi yake kwa mashabiki.

Leave your comment