Nyimbo Mpya: Zuchu ‘Mwambieni’, Harmonize ‘Mwaka Wangu’ na Ngoma Zingine Mpya Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

[Picha: Global Publishers]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ni wiki nyingine tena ambayo wasanii kutokea Tanzania wamezidi kuchangamsha soko la Bongo Fleva kwa kutoa ngoma kali zaidi. Bila shaka ngoma hizo zimezidi kuweka muziki huu wa Bongo Fleva kwenye sehemu nzuri. Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka nchini Tanzania kwa wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Ngoma Mpya ‘Mwaka Wangu’

Mwambieni - Zuchu

Mwanamuziki Zuchu amefungua ukurasa wa kimuziki kwa mwaka 2022 baada ya kuachia ‘Mwambieni’ ngoma ambayo ndani yake anatuma salamu kwa mpenzi wake wa zamani kuwa katu hawezi kurudiana nae na kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara laki tano themanini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=_QIvgJ0Hu8Y

As Long as you Know - Jux

Mwanamuziki Jux amezidi kuonesha umahiri wake kwenye muziki wa RnB kupitia ngoma yake ya ‘As long as you know’, kibao ambacho Jux anaimba kwa hisia sana akimsihi mwanadada ampendaye arudi kwake iwapo ataona huko alipo hapamfai.

https://www.youtube.com/watch?v=_Otneue_3Yo

Kidogo - Tommy Flavour

Mdundo mkali kutoka kwa mtayarishaji wa muziki Blaq pamoja na sauti tamu kutoka kwa Tommy Flavour ni moja ya vitu ambavyo vimefanya ‘Kidogo’ iwe ni ngoma kali sana. Muda mfupi tu tangu kuachiwa kwake kurindima vilivyo kwenye mitaa mbalimbali hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=oe2-n9MtRdA

Hellow - Baba Levo

Kama alivyoahidi mwaka jana, Baba Levo ameanza mwaka 2022 kwa kasi kubwa kwa kutoa ngoma mpya ya kuitwa ‘Hellow’ ambayo ni ngoma ya mapenzi itakayokufanya uzidi kumpenda na kumjali zaidi mpenzi wako pindi utakapoisikiliza.

https://www.youtube.com/watch?v=knQWPfw2v6Y

Mwaka Wangu - Harmonize

Harmonize amezidi kupeperusha vyema bendera ya Kondegang baada ya kuachia ‘Mwaka Wangu’. Hii ni ngoma ambayo imemleta Harmonize mpya ambaye ndani ya ngoma anaonesha jinsi anavyotamani kufanya mambo makubwa kwa mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=9Iu9eovU2V0

Leave your comment

Top stories