Harmonize Amtaka Alikiba Kuburudisha Siku ya Kumposa Mpenzi Wake

[Picha: East Africa TV]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Harmonize ameibua gumzo mtandaoni baada ya kuweka wazi kuwa angependa msanii nyota Alikiba kutumbuiza kwenye hafla ya kumposa mpenzi wake.

Harmonize aliandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram, alipokuwa akikula bata na mpenzi wake Brianna.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Tarehe ya Tamasha la Afro East Carnival

Bosi huyo wa lebo ya Konde Music World alikuwa akiusikiliza wimbo wa Alikiba unaofahamika kama ‘Utu’. Aliguswa mno na mistari ya wimbo huo na hivyo basi kuelekea kuupenda.

Ngoma ya ‘Utu’ ni moja kati ya ngoma kumi na sita ambazo zinapatikana kwenye Albamu ya Alikiba ya ‘Only One King’ iliyotoka mwaka jana.

"Someone tell the legend king, he must sing at my engagement night this dope music," Harmonize alisema katika chapisho aliloliweka mtandaoni.

Soma Pia:Nyimbo Mpya: Moni Centrozone Aachia EP Mpya ‘Road to Mazengo’ 

"This one, so pure music, so deep in this one," aliongezea kwenye chapisho lingine.

Kauli ya Harmonize imepokelewa na furaha tele na wadau tofauti kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania. Kauli hiyo ni dhibitisho kuwa Harmonize hana mgogoro wowote na Alikiba kama jinsi imekuwa ikidaiwa mtandaoni.

Hii pia imeonekana kuleta ukaribu na umoja miongoni mwa wasanii wa bongo. Mwaka jana, picha iliyomwonyesha Harmonize akiwa ameketi kando ya Alikiba kwenye ndege ilivuma sana mtandaoni.

Alikiba kwa upande mwingine hajatoa kauli yake kuhusu chapisho la Harmonize. Wawili hao ni mastaa wa muziki ndani na nje ya Tanzania.

Leave your comment

Top stories

More News