Nyimbo Mpya: Moni Centrozone Aachia EP Mpya ‘Road to Mazengo’

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Moni Centrozone ameachia EP mpya kabisa ambayo ameipa jina la ‘Road to Mazengo’

‘Road to Mazengo’ ni EP ambayo imesheheni ngoma tano na ndani yake amewashirikisha wasanii kama Young Lunya kwenye ‘Mama La Mama’, One Six kwenye ‘Shuka la Masai’ pamoja na Slimsal kwenye ‘458’, huku ngoma kama ‘Wrong Turn’ pamoja na ‘Show Killer’ akiwa amefanya peke yake.

Soma Pia: Mbosso Atangaza Kuachia Albamu Mwaka Huu

EP hii kutoka kwa Moni Centrozone ni mradi wake mkubwa zaidi tangu aanze muziki na inakuwa ni EP yake ya kwanza kuachia tangu ajiunge na lebo ya Rooftop Entertainment mwaka jana.

Kinachovutia zaidi kwenye EP hii ni namna ambavyo Moni ameweza kushirikisha watayarishaji wa muziki tofauti tofauti kutengeneza kazi.

Watayarishaji walioshiriki kwenye EP hii ni pamoja na Tracks, Slim Sal, Pol Maker, Tony Drizzy na S2kizzy ambaye ameshiriki kuandaa ngoma ya ‘Mama La Mama’.

Soma Pia: P Funk Majani Atangaza Tarehe ya Kuachia Albamu Yake

Kazi hii mpya kutoka kwa Moni inazidi kukoleza utaratibu wa wasanii wa Hip-hop nchini Tanzania kupendelea kutoa EP.

Mwezi Desemba mwaka 2021, Gnako aliachia EP yake ya kuitwa ‘Kitimoto’ na wiki mbili baadae rapa Conboi aliachia EP yake ya kuitwa ‘True Story’ ambayo ilifanya vizuri sana.

Leave your comment

Top stories

More News