P Funk Majani Atangaza Tarehe ya Kuachia Albamu Yake

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji nguli wa muziki kutokea nchini Tanzania P Funk Majani ametangaza kuwa albamu yake iko mbioni kukamilika na anatarajia kuiachia mwaka huu.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, mtayarishaji huyo ambaye amehudumu kwenye kiwanda cha muziki kwa takriban miaka 20 alitangaza kuwa asilimia 80% ya albamu hiyo imeshakamilika na anatarajia kuiachia Machi 30 mwaka huu.

Soma Pia: Director Ivan Azungumzia Kuchukua Nafasi ya Director Kenny Kwenye Zoom Extra ya Diamond

"My album ‘Majani’ is 80% complete, God willing we dropping on March 30 2021," aliandika P Funk kupitia akaunti yake ya Twitter.

Hii inatarajiwa kuwa albamu ya pili kuachiwa chini ya lebo hiyo ya Bongo Records kwani albamu ya kwanza kuachiwa chini ya uangalizi wa lebo hiyo ni ‘Wanangu 99’ ya kwake Rapcha.

P Funk anakuwa sio mtayarishaji wa muziki wa kwanza kutoka Tanzania kuachia albamu kwani mwaka 2021 mtayarishaji wa muziki nguli kutoka Tanzania Abbah Process aliachia albamu yake ya kuitwa ‘The Evolution’.

Soma Pia: Lava Lava Adokeza Ujio wa Ngoma yake Mpya 'Desh Desh'

‘The Evolution’ ilisheheni ngoma 16 huku akishirikisha wasanii wengi kama Jux, Maua Sama, Marioo, Nandy, Young Dee, Harmonize, Darassa na wengineo wengi.

Ikumbukwe kuwa P Funk Majani ni moja ya watayarishaji wa muziki wakongwe hapa nchini na ambaye ameshafanya kazi na wasanii wengi wakubwa kama vile Lady Jaydee, Juma Nature, AY, Solo Thang, Profesa Jay, Chege, Temba na wasanii wengine wengi.

Leave your comment