Director Ivan Azungumzia Kuchukua Nafasi ya Director Kenny Kwenye Zoom Extra ya Diamond

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muongozaji video kutoka nchini Tanzania Ivan hivi karibuni amekanusha tetesi zilizosambaa kuwa huenda yeye ndiye akawa director rasmi wa kampuni ya Zoom Extra inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Hapo awali, Director Kenny ndiye alikuwa director rasmi wa Zoom Extra na alihusika kuandaa video nyingi za Diamond Platnumz.

Baada ya Kenny kuacha kufanya kazi na Diamond, Ivan ndiye amehusika kuandaa video ya Diamond ya kuitwa ‘Unachezaje’, na tangu kuachiwa kwa video hiyo, kumekuwa na tetesi kuwa huenda yeye akakaimu nafasi ya Kenny kwenye kampuni hiyo ya Zoom Extra.

Soma Pia: Whozu Atangaza Kuachia Albamu Mwaka Huu

Akiongea kwenye mahojiano hivi karibuni, Ivan amefunguka kuwa kila mtu ana nafasi yake kwenye muziki na kwamba anaamini kabisa Kenny ana ubora wake na hayuko pale kwa ajili ya kuchukua nafasi yake.

"Haimaanishi kwamba mimi nitachukua nafasi ya mtu yeye atabakia na nafasi yake na mimi ntabakia na nafasi yangu. Kila mtu ana makali yake. Kenny ana makali yake, Hanscana ana makali yake na mimi nina makali yangu pia. Ni kuonesha watu ni kitu gani ambacho natakiwa kufanya na kustick sehemu ambayo unadhani hii inafaa," alizungumza Ivan.

Soma Pia: Lava Lava Adokeza Ujio wa Ngoma yake Mpya 'Desh Desh'

Aidha, kupitia mahojiano hayo, Ivan alieleza kuwa alijifunza mambo lukuki kipindi anafanya kazi na Diamond Platnumz kwenye ‘Naanzaje’ amabayo ilikuwa kazi yake ya kwanza kufanya na Diamond.

"Yeye Diamond ni mtu ambae amefanya video na madirectors wengi sana, wakubwa sana so anajua mistakes ambazo sisi watanzania tunakuwa tunazikosea. Mtu design kama ile akija akikwambia fanya hivi fanya hivi unakuwa unaelewa," alizungumza Ivan.

Leave your comment