Mbosso Atangaza Kuachia Albamu Mwaka Huu

[Picha: Mbosso Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutoka lebo ya WCB Mbosso amezidi kunogesha kiwanda cha Bongo Fleva baada ya kutangaza kuwa ataachia albamu mpya mwaka huu.

Mbosso ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Nigeria kwa sababu za kazi, amesema kuwa kwa sasa ana kazi nyingi sana ambazo ameshaziandaa hivyo mashabiki zake wategemee yeye kuachia albamu au hata EP kwa mwaka wa 2022.

Soma Pia: Mbosso Atangaza Ujio wa Kolabo Tano za Kimataifa

"Mwaka huu pia natarajia kutoa album lakini kama haitakuwa album basi itakuwa EP kwa sababu kazi zipo nyingi sana za sehemu tofauti tofauti. Tuna collabo na nchi tofauti tofauti. Namshukuru Mungu huu ni moja ya mwaka ambao watu watasikia sound ya tofauti sana kutoka kwangu," alizungumza Mbosso.

Iwapo Mbosso atatimiza ahadi yake ya kuachia albamu, basi albamu hiyo inatarajiwa kuwa ya pili kwa Mbosso baada ya ‘Definition of Love’ ya mwaka 2021 kuweza kufanya vizuri sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu ‘Mwambieni’, Harmonize ‘Mwaka Wangu’ na Ngoma Zingine Mpya Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Aidha, Mbosso alitumia fursa ya mahojiano hayo kueleza kuwa kipindi yupo nchini Nigeria amefanya collabo nyingi sana na wasanii wa nchi hiyo na hivyo mashabiki wategemee vitu vizuri.

"Safari ilikuwa ina manufaa makubwa sana kwa sababu mara ya mwisho kwenda Nigeria ilikuwa 2019 nilienda kwa ajili ya tuzo za Afrimma nikarudi. Safari hii nilienda kwa ajili ya kujizatiti na kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti kuandaa kazi zangu mimi ukiachilia mbali hizo collabo," alizungumza Mbosso.

Leave your comment

Top stories

More News