Billnass Aeleza Sababu Yake Kufanya Muziki wa Amapiano

[Picha: Millard Ayo]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Billnass hatimaye ameeleza kwa uwazi sababu gani hasa zilizopelekea yeye kufanya muziki wenye mahadhi ya Amapiano.

Billnass ambaye anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kuandika ngoma za Hiphop, kwenye ngoma zake mbili za mwisho ambazo ni ‘Tit For Tat’ pamoja na ‘Chetu’ alipita kwenye mdundo wa Amapiano kitu ambacho kilileta taharuki kwa mashabiki kuhusu sababu gani haza zilizofanya Billnass afanye muziki huo.

Soma Pia: Mbosso Atangaza Ujio wa Kolabo Tano za Kimataifa

Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, Bilnass amefunguka kuwa aliamua kufululiza kufanya Amapiano ili ngoma zake ziweze kusikika na watu tofauti tofauti kwenye maeneo mbalimbali.

"Sababu ya kufululiza kutoa ile Amapiano ni kutengeneza pia playlist nyingine yani kuweza kuwa katika kila sehemu. Watu wasikilize aina ya muziki lakini wakiwa sehemu nyingine pia wananisikia" alizungumza Billnass.

"Kwa hiyo ni kutengeneza tu varieties, ukiwa club utamsikiliza Billnass, ukiwa sad pia unaweza ukamsikiliza Billnass. Pia ukiwa unambembeleza mpenzi wako unaweza ukasikiliza pia wimbo. Yaani naongeza varieties za muziki," msanii huyo aliongezea.

Soma Pia: Lava Lava Adokeza Ujio wa Ngoma yake Mpya 'Desh Desh'

Kauli ya Billnass bila shaka itaungwa mkono na wasanii kama Zuchu, Whozu, Harmonize, Rayvanny, Diamond Platnumz, Damian Soul na Mwasiti ambao wao pia wameshaachia ngoma ambazo zina mdundo wa Amapiano wakisisitiza kuwa ni muziki wa Afrika na katu hauwezi kuua Bongo Fleva.

Aidha wasanii na wadau wengine wa muziki kutoka Afrika Mashariki kama Eric Omondi pamoja na AY wameonekana kutopendezwa na hulka ya wasanii wa Bongo kupendelea kufanya Amapiano.

Leave your comment

Top stories

More News