Young Dee Afungua Studio Yake

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Young Dee amepiga hatua nyingine kwenye muziki wake baada ya kufungua studio yake ya kisasa aliyoipa jina la Dream City.

Young Dee ambaye kwa mwaka 2021 aliachia albamu yake ya kuitwa ‘Nyanguva’, alitangaza kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa studio yake iko tayari na kwamba wasanii na watengeneza maudhui wanakaribishwa kwa ajili ya kufanya kazi.

Soma Pia: Conboi Aeleza Anavyojisikia Akifananishwa na Young Lunya

Kwenye taarifa hiyo, Young Dee alipambanua kuwa studio yake haipo kwa ajili ya wanamuziki pekee bali inafanya kazi na kurekodi vipindi vya redio, matangazo, tamthiliya na maudhui mengine mengi.

Aliongeza kuwa yupo tayari kupokea wazo lolote linalohusu maudhui kwa njia ya sauti.

"Dream City HQ iko live now. Tunarekodi Muziki | Matangazo | Soundtrack za Vipindi na Tamthiliya | Radio Drama | Vipindi vya Radio | Pia kama una idea yoyote inayohusu programs za Sauti (audio) na unahitaji kufanya biashara ya maudhui ya sauti milango ipo wazi kwa ajili ya partnership | Ushirikiano au ushauri na kufanya biashara pamoja," aliandika Young Dee.

Soma Pia: Tommy Flavour Athibitisha Albamu Yake Kusheheni Wasanii wa Kimataifa

Kufikia sasa, bado Young Dee hajamtambulisha mtayarishaji wa muziki rasmi kwa ajili ya studio hiyo ambayo inatarajiwa kuwa ni moja ya studio ya kutegemewa sana kwa hapa nchini Tanzania.

Kando na Young Dee, wasanii wengine ambao wanamiliki studio zao hapa nchini Tanzania ni pamoja na Diamond Platnumz anayemiliki Wasafi Records, Nahreel wa The Industry pamoja na Barnaba ambaye anamiliki studio yake ya kuitwa ‘High Table Sounds’.

Leave your comment