Tommy Flavour Athibitisha Albamu Yake Kusheheni Wasanii wa Kimataifa

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkali wa RnB kutokea nchini Tanzania Tommy Flavour hivi karibuni amethibitisha kuwa albamu yake ya kuitwa ‘Heir To The Throne’ ambayo iko mbioni kuingia sokoni itasheheni collabo za wasanii wa kimataifa.

Akiongea kwenye kipindi cha Empire, Tommy Flavor alidokeza kuwa albamu yake imejaa collabo za kimataifa kuanzia wasanii wa ndani ya Afrika kama nchini Kenya na hata wa nje ya bara la Afrika pia wapo kwenye albamu hiyo.

"Wapo kutoka Kenya ambao tumefanya nao wengine nje ya Afrika, wengine nchi za hapa hapa Afrika kwa hiyo iko vizuri ina utofauti ina kile kitu ambacho nafikiri mashabiki wangu walikuwa wanakihitaji kwa muda mrefu," alizungumza Tommy Flavour.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘Lay Down’ na ‘Kidogo’

Aidha, Tommy Flavour hakutaka kuweka wazi tarehe ambayo anaachia albamu hiyo au wasanii ambao wanatarajiwa kushiriki kwenye albamu hiyo.

Alabamu yake inatarajiwa kuwa albamu ya pili kuachiwa tangu kuanzishwa kwa lebo ya King's Music, baada ya albamu ya Ali Kiba ya ‘Only One King’ kuingia sokoni mwezi Oktoba mwaka jana.

Soma Pia: Tommy Flavour Apinga Vikali Mahusiano Katili

Kando na Tommy Flavour wasanii wengine ambao wanatarajiwa kuachia albamu kwa mwaka huu ni pamoja na Rosa Ree, Ibraah, Marioo, Diamond pamoja na Young Lunya ambaye kwa muda mrefu kupitia vyombo vya habari alitangaza kuwa anaweza kuachia albamu.

Leave your comment