Conboi Aeleza Anavyojisikia Akifananishwa na Young Lunya

[Picha: Conboi Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Conboi hivi karibuni amefunguka namna anavyojisikia pale ambapo mashabiki wanamfananisha kimuziki na rapa mwenzake Young Lunya.

Conboi ambaye kwa sasa hivi anatamba na EP yake ya ‘True Story’ aliyoiachia mwezi Desemba mwaka 2021, akiwa kwenye mahojiano kwenye kipindi cha XXL alifafanua kuwa anaheshimu maoni ya kila mtu na kwamba anachukulia kawaida tu kufananishwa na Young Lunya.

Soma Pia: AY Azungumzia Muziki wa Amapiano Kupata Umaarufu Tanzania

"Siichukulii vyovyote naichukulia kama perspective za watu tofauti tofauti kwa sababu kila mtu ana mawazo yake mimi I don’t take it personal nnavyoona watakavyojadili watu nikikutanayo. I'll just laugh coz pengine yanachekesha," alisema Conboi.

Ikumbukwe kabla hajaanza kufanya muziki kama msanii binafsi, Conboi alikuwa na Young Lunya pamoja na Salmin Swaggz kwenye kundi moja la Hip-hop la kuitwa OMG, kundi ambalo lilipata umaarufu mkubwa mwaka 2017 kabla ya kuvunjika mwaka 2020.

Tangu kuvunjika kwa kundi hilo, wengi wamekuwa wakiwashindanisha Young Lunya na Conboi. Akizungumzia uhusiano uliopo kwa sasa kati ya wasanii hao watatu waliokuwa wakiunda kundi hilo, Conboi alidokeza kuwa pamoja na kwamba hawakutani mara kwa mara lakini uhusiano wake na Young Lunya pamoja na Salmin Swaggz uko vizuri na hawana ugomvi.

Soma Pia: Harmonize Adokeza Nia ya Kufanya Collabo na Tunda Man

"Sasa hivi tunafanya kazi, solo project kila mtu anajitegemea, yani tuko vizuri ubaya ni kwamba tunaweza tusiwasiliane lakini there is still love yaani we don't have to talk about it. We may not speak lakini still love yaani mi i feel love," alizungumza Conboi.

Leave your comment