Nyimbo Mpya: Jux Aachia ‘As Long As You Know’

[Picha: Jux Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Jux ameachia ngoma mpya kwa jina la ‘As Long As You Know’.

Ngoma hiyo inazungumzia hali ya mhusika, ambaye ni Jux, kumpenda mwanamke ambaye yupo kwenye mahusiano na mtu mwingine. Mwanamke huyo, hata hivyo, hana furaha kwenye mahusiano hayo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘Lay Down’ na ‘Kidogo’

Jux kupitia wimbo huu anamwambia kuwa si lazima awe naye ila cha muhimu ni ajue jinsi anvyohisi.

"Hauna furaha, Haifichi sura yako. Najua una mpenzi, Unampenda ila moyo wako haupo hapo. Unapata karaa Unatunza utu wako (Mmm) Labda unajiuliza kwanini nahitaji namba yako. (Ilaaa). Sio lazima nikipiga simu upokee (Aa aa aa aaah) Sio lazima message zangu majibu yarejee (Aaa aaa aaah aah) Nasema sio lazima mi nawe tukae tuongee (Ilaaa) Ukipata muda (Majiii) yakizidi unga nipigie," Jux anaimba katika kipande cha ngoma hiyo.

Soma Pia: Killy Atangaza Ujio wa EP Yake ‘The Greenlight’

Ngoma hiyo imesukwa na kutayarishwa na Foxx Made It. Mdundo wa ngoma hiyo unaendana na maudhui yake ya mapenzi.

Jux amesifiwa sana kwa ustadi wake wa kutunga na kuimba nyimbo za mapenzi haswaa zenye hisia nzito. Japo video rasmi bado haijatoka, ngoma hiyo imepokelewa vyema na mashabiki na imesikizwa na maelfu ya mashabiki kwenye mtandao wa YouTube. K

wa sasa mashabiki wanasubiri msanii huyo aachie video rasmi ya ngoma hiyo. Jux hajadokeza tarehe rasmi ya kuachia video.

https://www.youtube.com/watch?v=_Otneue_3Yo

Leave your comment