Killy Atangaza Ujio wa EP Yake ‘The Greenlight’
18 January 2022
[Picha: Side Makini]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki kutokea himaya ya Konde Music Worldwide Killy kwa mara nyingine amechangamsha kiwanda cha Bongo Fleva baada ya kutangaza kuachia EP yake ya kwanza tangu aanze muziki aliyoipa jina la ‘The Greenlight’.
Killy ambaye kwa sasa anatikisa Afrika Mashariki na video ya ngoma yake ya ‘Ni Wewe’ alitangaza ujio wa mradi huo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo aliwashukuru watu wote walioshiriki kuandaa EP hiyo iliyosheheni ngoma tano.
Soma Pia: Killy Ataja Producer Anayemkubali Zaidi Tanzania
Wasanii ambao wameshirikishwa kwenye EP hiyo ni Ibraah aliyeshiriki kwenye ‘Kiuno’ na Christian Bella ambaye ameshiriki kwenye ngoma ya ‘Niambie’.
Ngoma nyingine zote kama ‘Vumilia’, ‘Itafika’ pamoja na ‘Ilete’ Killy amefanya peke yake.
Aidha, Killy pia aliwashukuru watayarishaji wa muziki watatu ambao ni Mocco Genius, Wambaga pamoja na Terriyo Monster kwa kuweza kushiriki kikamilifu kwenye EP hiyo ambayo alitanabaisha ametumia muda mwingi sana kuiandaa.
Soma Pia: Killy ‘Ni Wewe’, Diamond ‘Unachezaje’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Tanzania Wiki Hii
"Shukrani nyingi pia ziwaendee maproducer tulioshirikiana kutengeneza hizi nyimbo Terriyo Monster, Mocco Genius, Wambaga na wasanii wenzangu nilioshirikiana nao kukamilisha ep yangu ya kwanza kabisa The Greenlight EP. Pamoja na management yangu nzima ya Konde Gang bila kumsahau boss wangu Harmonize," aliandika Killy.
Killy anatarajiwa kuwa msanii wa pili kutokea Konde Gang kuachia EP yake tangu kuanzishwa kwa lebo hiyo, msanii wa kwanza akiwa ni Ibraah alipoachia EP yake ya ‘Steps’ mwaka 2020 na EP ya pili ya kuitwa ‘Karata Tatu’ aliiachia Januari mwaka 2021.
Leave your comment