Killy ‘Ni Wewe’, Diamond ‘Unachezaje’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii kutokea Tanzania wameendelea kuachia ngoma kali kupitia mtandao wa YouTube na bila shaka mashabiki wamekuwa kama waamuzi wa kuchagua ni ngoma gani ipande na ngoma gani ishuke kwenye mtandao huo. Hivyo basi zifuatazo ni orodha ya ngoma tano ambazo zinafanya vizuri zaidi nchini Tanzania kwenye mtandao wa YouTube:

Soma Pia: Diamond Platinumz Adokeza Ujio Mpya Wa Queen Darleen

 Why - The Ben ft Diamond Platnumz

Ngoma hii imezidi kufanya vyema huko YouTube na hii ni kutokana na kuwa na ujumbe mzuri na hata video yake inavutia sana hivyo kupelekea wana Afrika Mashariki kuipenda. Kufikia sasa, video hio imeshatazamwa mara Milioni 2.3 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=10tGnm2h9qQ

Unachezaje - Diamond Platnumz

Ngoma hii ambayo imesheheni mitindo tofauti tofauti ya dansi kutoka kwa Diamond Platnumz, kwa wiki ya pili mfululizo imeendelea kusumbua kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 3.2 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=Y8n1qpw7Ijw

Ni Wewe - Killy ft Harmonize

Ngoma ya ‘Ni Wewe’ imeweza kupata mafanikio makubwa huko YouTube na huenda hii ni kutokana na video hii kusubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wa muziki. Kufikia sasa, video hio imeshatazamwa mara laki saba na elfu hamsini na tisa ndani ya siku moja tu.

https://www.youtube.com/watch?v=CRcm6EeFPNI

Serious Love – Harmonize

Tangu kuachiwa kwake, ‘Serious Love’ imekuwa ni ngoma pendwa hasa kwa wapendanao kutokana na mashahiri yake kugusa.  Video ya ngoma hii imeshatazamwa mara laki nane arobaini na tisa kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=59jN0K1n7ZM

Tausi - Mrisho Mpoto ft Mbosso

Kwenye ngoma hii Mbosso anamsifia na kumpa sifa nyingi mpenzi wake huku Mrisho Mpoto ametumia kwa wingi lugha ya picha pamoja na ubunifu mkubwa kwenye kujenga mashahiri ya ngoma hiii. Video ya ngoma hii bado haijaachiwa.

https://www.youtube.com/watch?v=GKtz_kLRWVA

Leave your comment