Killy Ataja Producer Anayemkubali Zaidi Tanzania

[Picha: Killy Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota kutokea Konde Gang Killy hivi karibuni ametaja mtayarishaji muziki anayemkubalii zaidi hapa nchini Tanzania.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari hapa nchini Tanzania, Killy amemtaja Terriyo Monster kama mtayarishaji bora wa muziki kwa upande wake.

Soma Pia: Belle 9 Aweka Wazi Msimamo Wake Kuhusu Kujiunga na Wasafi, Konde Gang au Kings Music

Killy alisema kuwa Terriyo Monster ni mojawapo ya watu wanaotengeneza muziki mzuri na anategemea siku za usoni mtayarishaji huyo atazidi kung'aa zaidi kwenye soko la muziki.

"Terriyo master ni producer mpya kwenye industry lakini namuona mbali miaka miwili mitatu hapo mbele atakuwa producer mkubwa sana. Terriyo ana uwezo mkubwa pengine anawazidi hata hao maproducer wakubwa waliopo kwenye industry. This time nadhani ni muda wake watanzania au mashabiki wa muziki kumfahamu,"alizungumza Killy.

Soma Pia: Tommy Flavor Afichua Sababu ya Kuandika Ngoma ya ‘Jah Jah’

Ukali wa Terriyo Master kwenye kuandaa midundo ya Bongo Fleva unaonekana dhahiri shahiri kwenye ngoma ya ‘Roho’ ya msanii Killy.

Aidha, Killy pia alimtaja Mocco Genius kama mtayarishaji mwingine wa muziki anayefanya vizuri zaidi nchini Tanzania. Killy alimsifu Mocco Genius kwa kuweza kumpika Terriyo Master vizuri mpaka akawa mtayarishaji nguli wa muziki nchini Tanzania.

Tangu aingie Konde Gang, Killy tayari ameshafanya kazi na watayarishaji muziki watatu ambao ni Terriyo Master kwenye ‘Roho’, Neksazy kwenye ‘Mwisho’ pamoja na ‘Hunter’ kwenye ‘Ni Wewe’ kibao ambacho ameshirikiana na Harmonize.

Leave your comment