Alikiba Amtaja Producer Yogo Kama Mtayarishaji Bora Wa Muziki

[Picha: Wikimedia]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki wa bongo Alikiba amemtaja Producer Yogo kama mtayarishaji bora wa muziki.

Alikiba aliweka hili wazi kupitia ukurasa wake wa kijamii. Kauli ya Alikiba iliibua mjadala mkubwa katika sehemu ya maoni ya chapisho lake.

Soma Pia: Lebo Tano Kutoka Tanzania Zinazotarajiwa Kufanya Vizuri Mwaka 2022

Wapo mashabiki ambao walikubaliana naye, ila wengine walimpinga kwa kusema kuwa wapo watayarishaji wa muziki ambao wanafanya kazi nzuri zaidi. Idadi kubwa ya mashabiki hata hivyo walimpa Producer Yogo heshima kwa kazi na mchango wake kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania.

Producer Yogo kwa siku za hivi karibuni amekua gumzo sana mtandaoni baada ya albamu ya Alikiba ya 'Only One King' kupata mapokezi mazuri. Nyimbo zote kumi na sita kwenye albamu hiyo zilitayarishwa na Producer Yogo; jambo ambalo si la kawaida kwenye muziki.

Soma Pia: Producer Bonga Atangaza Kufanya Kazi na Konde Gang

Mara mingi, albamu huwahusisha watayarishaji wa muziki tofauti ili kuleta ladha tofauti ya midundo. 'Only One King' hata hivyo ilitayarishwa na Producer Yogo pekee. Licha ya kuwa ilikua kazi kubwa na yenye uhitaji wa ustadi mkubwa, Producer Yogo alimfanyia Alikiba haki, kwani ngoma mingi kwenye albamu hiyo zilikubaliwa na mashabiki.

Producer Yogo, vile vile, amekua akifanya kazi na Alikiba kwa muda mrefu sana. Kando na albamu hiyo, Producer Yogo ametayarisha ngoma mingi za Alikiba ambazo zilipata mafanikio makubwa mno.

Leave your comment