Paul Maker Atangaza Kuachia Albamu Mwaka Huu

[Picha: PaulMaker Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa mashuhuri kutokea nchini Tanzania Paul Maker hivi karibuni ametangaza kwa mashabiki zake kuwa anatarajia kutoa albamu yake ndani ya mwaka huu wa 2022.

Paul Maker ambaye ukiachana na talanta yake yake kwenye muziki wa Hiphop ni mtayarishaji wa muziki nguli nchini Tanzania, ametoa tangazo hilo ikiwa ni zaidi ya miezi sita imepita tangu aachie ngoma yake ya ‘Instructions’ ambayo ilifanya vizuri sana.

Soma Pia: Sallam SK Azungumzia Uhaba Wa Usimamizi Mzuri wa Wasanii Tanzania

Akiongea kwenye kituo cha redio cha Times FM, Paul Maker alidokeza kuwa yupo mbioni kuachia albamu mwaka huu na hivyo mashabiki zake wakae mkao wa kula pindi wanaposubiri albamu hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza tangu aanze muziki.

"Mashabiki zangu wategemee kitu kikubwa sana mwaka 2022 sababu nataka nitoe albamu, ntatoa albamu yangu ambayo pia itajulisha nyimbo zangu nilizotoa mwanzo kama ‘Serikali Kuu’ na ‘Instructions’,” alidokeza msanii huyo ambaye ana ukaribu mkubwa sana na rapa Young Lunya.

Aidha, Paul Maker alizidi kudokeza kuwa kabla hajaachia albamu hiyo ataanza kwa kuachia ngoma nyingine kwanza kama ambavyo alikuwa anafanya hapo mwanzo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Ya ‘Rara’

"Ila before nitarelease nyimbo nyingine pia kama vile nilivyokuwa nafanya so 2022 naamini ntaachieve vitu vikubwa sana," alizungumza rapa huyo.

Taarifa hii kutoka kwa Paul Maker imezidi kuonesha mwamko wa wasanii wa Hiphop katika kuachia albamu. Kando na rapa huyu, pia Young Lunya aliahidi kutoa albamu toka mwaka 2021 na pia Rosa Ree aliahidi kuwa ndani ya mwaka 2022 ataachia albamu yake.

Leave your comment