Alikiba Adokeza Ujio wa Albamu Mpya Mwaka wa 2022

[Picha: Africa Billboard]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mfalme wa muziki wa bongo Alikiba amedokeza ujio wa albamu mpya mwaka huu wa 2022.

Alikiba alifichua habari hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii. Msanii huyo hata hivyo hakutaja tarehe kamili ya albamu hiyo kutoka wala habari yoyote kuhusu utayarishaji wake.

Soma Pia: Alikiba Adokeza Kuachia Ngoma Mpya Mbili Hivi Karibuni

"Thinking of releasing another album 2022," chapisho la Alikiba mtandaoni lilisomeka.

Kauli hiyo kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa lebo ya Kings music inatokea miezi michache tu baada ya yeye kuachia albamu ya 'Only One King' ambayo ilikuwa na nyimbo kumi na sita.

Albamu hiyo ilitayarishwa na mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania Producer Yogo. Yogo alihusika katika kusuka midundo zote kwenye albamu ya 'Only One King'. Albamu hii ilikuwa na utofauti mkubwa sana na albamu nyingine za Alikiba. Hii ni kutokana na Alikiba kufanya kazi na wasanii wengi kutoka mataifa mbali mbali.

Soma Pia: Zuchu, Barnaba Wapinga Madai ya Muziki wa Bongo Kufa

Alikiba alieleza kuwa alifanya makusudi kuwahusisha wasanii tofauti kwenye albamu hiyo kwa ajili ya mashabiki wake. 'Only One King' ilipata mapokezi mazuri sana si Tanzania tu bali barani Afrika.

Kupitia albamu hiyo, Alikiba alizindua 'Only One King Tour' ambayo ilimpeleka hadi nchini Kenya alikotumbuiza. Ziara hiyo ya muziki iliwavutia mastaa mbali mbali kwenye tasnia ya muziki ikiwemo nyota wa muziki kutoka nchini Kenya Otile Brown. Ni kupitia ziara hiyo ndio Otile Brown alitumbuiza nchini Tanzania kwa mara ya kwanza kabisa.

Leave your comment