Lulu Diva Aomboleza Kifo cha Mamake

[Picha: Lulu Diva Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka Tanzania Lulu Diva anaomboleza kifo cha mamake ambaye aliaga dunia mnamo tarehe 19 mwezi huu wa Disemba. Msiba huo umetokea takriban miezi miwili na nusu tangu mamake Lulu Diva ashereheke siku yake ya kuzaliwa akiwa amefikisha miaka sitini.

Kabla ya kifo chake, mamake Lulu Diva alikuwa ameugua kwa muda mrefu sana. Lulu Diva kupita mtandao wa kijamii amekuwa akichapisha picha za mamake na kumtakia nafuu.

Soma Pia: Matamasha ya Muziki Tanzania Yaliyofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

 Ikumbukwe kuwa mwezi wa nne mwaka huu, Lulu Diva aliacha wimbo uliopewa jina la 'Mama'. Wimbo huo alimuimbia mamake ambaye pia alionekana kwenye video yake.

Wakati mamake anasheherekea kuitimisha miaka sitini, Lulu Diva alichapisha ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake ambapo alimsifia mno. Kwenye ujumbe huo, Lulu alimshukuru Mungu kwa kumweka mamake hai. Vile vile alionyesha kwa jinsi gani anampenda mno.

Soma Pia: Collabo 10 Kali Kutoka Tanzania Zilizofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

"Happy Birthday my dear mum, my life partner alhamdulilah alhamdulilah alhamdulilah nina kila sababu ya kumshukuru Allah si kwamba mimi ni wapekee sana kuendelea kunilindia ww ambae ni furaha yangu ya maisha hapana bali ni baraka zake na ukuu wake mama angu namshukuru mungu kwakuendelea kua na mimi haijalishi unapitia nini imani yangu ipo siku utaamka tena na utaniita jina langu nakufurahia vile vichache kati ya vingi tulivyokua tukipiga magoti kwa pamoja tukiomba allah atubariki” kwa kidogo nilichopata hata uwezo kwa uwezo wangu huu mdogo nataman kukupa kila utakacho," kipande cha chapisho la lulu diva kilisomeka.

 Mashabiki wamejiunga na Lulu Diva katika kuomboleza kifo cha mamake na kumtakia nguvu pamoja na uvumilizi katika wakati huu mgumu.

Leave your comment