Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video ya 'Ng'ari Ng'ari
16 December 2021

[Picha: Citi Muzik]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Msanii tajika kutoka Tanzania LavaLava ameachia videoya wimbo wake mpya 'Ng'ari Ng'ari'.
Ngoma hii inasimulia hadithi ya mhusika ambaye anapata furaha tele kutokana na mapenzi ya dhati anayopata.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Kayumba Aachia Video ya ‘Mapenzi Yanauma’
Mapenzi haya hayana doa lolote na ndio maana Lava Lava akaupa wimbo jina la 'Ng'ari Ng'ari'.
Lava Lava pia kwa kiasi kwenye wimbo huo anasimulia jinsi alipitia maumivu katika mahusiano yake ya zamani. Ngoma hii vile vile inaguzia maudhui ya mapenzi katika dini tofauti.
Walioshiriki kwenye video wamevaa uhusika wa dini ya Kihindi. "Na nimeamua sitaki sitaki Kurudia matapishi nishakula yamini divai. Aende akanishitaki mahakamani polisi. Kama kuna kitu ananiclai Ooh poleni wanokonoko. Penzi linameta meta meta. Mwali fund si kitoto Kama kasomea veto veto. Mwiteni na kiroboto," Lava Lava anaimba kwenye kipande cha wimbo huo.
Mdundo wa 'Ng'ari Ng'ari' umetayarishwa na Lizer Classic kutoka lebo ya WCB. Video ya wimbo huu imeelekezwa na mwelekezaji wa video ambaye anafahamika kama Ivan.
Kilichowapendeza mashabiki wengi kuhusu video hii nii jinsi imerekodiwa katika mazingira ya unyenyekevu ambayo sio ya kitajiri.
Weekly Top 10 songs

Kamwambie3:47
chile-one-so-lucky4:02
Buwooma2:44
Joy Is Coming3:08
Nakupenda3:12
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Paver2:55
Ssirivawo ft yven feiz2:10
Ziyakuba kabotu6:57
Top stories
- One and only
01 May
- SHUKRANI
02 May
- Jaxon Ryker Official profile
30 April


Leave your comment