Orodha ya Wasanii Watakoitumbuiza Kwenye 'Only One King Tour' ya Alikiba

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mfalme wa muziki wa bongo Alikiba hivi karibuni atatumbuiza kwenye ziara yake ya muziki ya 'Only One King Tour' mjini Mwanza mnamo tarehe 17 mwezi huu wa Disemba.

Baada ya kupeleka ziara hiyo nchini Kenya kwenye hafla ya Afro-Vasha ambako alitumbuiza pamoja na wasanii wengine maarufu kama vile Willy Paul, Femi One, Nyashinski na wengine wengi, sasa ni zamu ya mashabiki wake wa Mwanza kupata kidonge chao cha burudani.

Soma Pia: Alikiba Afunguka Sababu ya Kutoiga Biashara ya Diamond

Kwa sasa msanii huyo ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Kings Music, anaendelea kufichua majina ya wasanii ambao watajumuika naye kwenye jukwaa.

Otile Brown kutoka nchini Kenya ni miongoni mwa wasanii ambao wataburudisha Mwanza. Otile ni mmoja kati ya wasanii ambao wako na ukaribu mno na Alikiba na hata washawahi kushirikiana kwenye ngoma iliyopewa jina la 'In Love'.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Ujio wa ‘Only One King’ Tour

Maua Sama ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya 'Baba Jeni' vile vile atakuwepo kwenye hafla hiyo. Ikumbukwe kuwa Maua Sama alirudi kwenye muziki wiki chache zilizopita baada yake kuugua kwa muda mrefu.

Abdu Kiba ambaye pia ni kakake mdogo wa Alikiba na vile vile mwanachama katika lebo ya Kings Music atapanda pia jukwaani kuwapa mashabiki burudani.

Mkongwe wa muziki wa Hip Hop Tanzania Mwana Flasafa au ukipenda Mwana FA pia ametajwa na amealikwa kwenye hafla hiyo kutumbuiza. Wasanii wengine ambao pia wametajwa ni pamoja na; K2ga, Rich Mavoko na Tommy Flavour.

Leave your comment