Joh Makini Azungumzia Bifu Kati ya Motra The Future na Mex Cortez

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kwa sasa kwenye kiwanda cha muziki hapa nchini Tanzania, mojawapo kati ya habari kubwa sana kwenye ni bifu uliopo kati ya rapa Motra The Future pamoja na Mex Cortez.

Mgogoro kati ya Motra The Future na Mex Cortez ulichipuka takribani wiki moja iliyopita baada ya Motra kuachia ngoma yake ya ‘Weupe’, ambayo ndani yake alitoa maneno ya kashfa kwa kikundi cha Kikosi Kazi ambacho kwa muda mrefu kimekuwa na utofauti na Weusi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Ng’ari Ng’ari’, Stamina ‘Paradiso’ na Ngoma Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Siku tatu baadae, Mex Cortez alitoa ngoma ya ‘Amkia’ ikiwa ni maalum kwa ajili ya kumjibu Motra The Future.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL, rapa Joh Makini kutokea kundi la Weusi; kikundi cha Hip-hop ambacho pia kimetajwa kwenye mgogoro huu, rapa huyo ametanabaisha kuwa kwake yeye anawapongeza wasanii wote wawili yaani Mex pamoja na Motra kwa kuweza kushika umakini wa watanzania kwa hivi karibuni.

"Mi nafikiri kwa kinachoendelea kwanza ni kitu poa kwa vijana kwa sababu mtaa unawasikiliza sasa hivi, mtaa unamsikiliza Motra mtu ambaye amekuwa kwenye game kidogo kwa muda na amekuwa akipigania nafasi yake kwa hiyo kuona msanii kama Motra anapata nafasi anayoipata sasa hivi kwenye game its a good thing," alizungumza Joh Makini.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Stamina Adondosha Video ya Wimbo wake 'Paradiso' amshirikisha Marissa

Aidha, Joh Makini alitumia mahojiano hayo kumshauri Motra kuwa atumie muda huu ambao watanzania wanamsikiliza na kumfuatilia kutengeneza kazi nzuri ili aweze kukuza jina lake zaidi kwenye muziki wa Bongo Fleva.

"Tayari watu wanawasikiliza watu wamepay attention kwa hiyo kilichobaki sasa ni inabidi wajipange kucome up na vitu ambavyo sasa vitashikilia kuanzia pale walipofikia kwenda mbele kwa hiyo mwanzo mzuri," alizungumza Joh Makini.

Leave your comment