Marioo Apinga Dhana Kuwa Muziki wa Bongo Fleva Umeshuka

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri kutokea Tanzania Marioo amepinga vikali dhana iliyopo kwa sasa kuwa muziki wa Bongo umeshuka viwango.

Kwa miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki nchini Tanzania kuwa muziki wa Bongo unapotea na kushuka, kutokana na wasanii wengi wakubwa kukumbatia muziki kutokea nchi za nje kama Amapiano na Kazomba.

Soma Pia: Marioo Azungumzia Tuhuma za Wasanii wa Bongo Kuiga Wimbo Wake ‘Beer Tamu’

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, Marioo alifafanua kuwa kwa upande wake, yeye haoni kama muziki wa Tanzania umeshuka bali hayo ni maoni tu ya watu.

"Kama kuna watu wanasema hivyo, lisemwalo lipo lakini kiukweli kwa upande wangu nipo kwa ajili ya kufanya muendelezo. Kama game ya Bongo Fleva itakuwa haiendi vizuri sijui itashuka na nini mi pia ntaumia sababu mi pia nategemewa. Hiyo comment ndo mimi siitaki game yetu imeshuka na nini na nini thats why tunafanya vitu tofauti tofauti, " alizungumza Marioo.

Kauli hii ya Marioo imekuja kwenye kipindi ambacho kuna sintofahamu kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania kuwa wasanii wanaacha kufanya muziki wa nyumbani na kukimbilia Amapiano au muziki wa nje.

Soma Pia: Marioo Amuunga Mkono Eric Omondi Kutaka Wasanii Wabongo Waheshimiwe

Kwa upande wa Marioo, kufikia sasa ameshaachia mikwaju miwili ya Amapiano ambayo ni ‘Mama Amina’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2020 pamoja na ‘Bia Tamu’ ya mwaka huu.

Leave your comment