Marioo Amuunga Mkono Eric Omondi Kutaka Wasanii Wabongo Waheshimiwe

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika kutoka Tanzania Marioo ameunga mkono hoja ya mchekeshaji kutokea Kenya kuhusu hali ilivyo kwenye soko la muziki nchini Tanzania.

Mnamo Novemba 6, mchekeshaji Eric Omondi alitetemesha kiwanda cha muziki nchini Kenya baada ya kudokeza kuwa wasanii wa nje wanapata hadhi kubwa kuliko wasanii wa Kenya na kwamba kiwanda cha muziki nchini Kenya kiko mahututi.

Soma Pia: Marioo Azungumzia Tuhuma za Wasanii wa Bongo Kuiga Wimbo Wake ‘Beer Tamu’

Chapisho hilo kutoka kwa Eric Omondi limeungwa mkono na Marioo ambaye amesema kuwa wasanii wakubwa kutoka Tanzania aghalabu huepuka kuwaunga mkono wasanii wengine hasa wale wachanga na hali hiyo inamuumiza sana

"Af chengine kinachoumiza ni hata hawa kaka zetu yaani hawatakagi kabisa kutusupport vijana wao unakuta wanaona bora wawape mashavu maunderground wa Nigeria au South kuliko sisi ambao tunahitaji baraka zao," aliandika Marioo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Soma Pia: Marioo Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina ili Kufanikiwa Kimuziki

Kwenye chapisho jingine, Marioo aliendelea kutoa ya moyoni kuhusu waandaaji wa matamasha kwa kusema kuwa wasanii kutoka mataifa ya nje pindi wanapokuja Tanzania hupewa hadhi na thamani zaidi kuliko wasanii wakubwa wa ndani.

"Sema hii kitu hata kwetu ipo Eric Omondi af inakata sana unakuta anakuja msanii kutoka Nigeria au South huko ana wimbo wake mmoja tu af unaweza kuta hata watu hawaujui ila treatment yake utafkiri wanataka kufunga nae ndoa af wasanii wao wanatuchukulia baridi baridi tu. Yaani sisi huku bongo wageni 90% af sisi 10% hii kitu imekaa kimiyeyusho sana," aliandika Marioo.

Suala la wasanii wa nyumbani kutopewa thamani sio suala geni sana hapa Afrika Mashariki kwani mwaka 2017 mwanamuziki kutoka Uganda Jose Chameleone alikataa kupanda jukwaani kwenye tamasha moja huko Uganda, baada ya picha ya Wizkid kuwekwa kwa ukubwa zaidi kuliko picha yake kwenye bango ambalo lilikuwa linatangaza tamasha hilo.

Leave your comment