Stamina Azungumzia Mapokezi ya Albamu Yake ‘Paradiso’

[Picha: Global Publishers]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea Tanzania Stamina ameweka wazi namna ambavyo albamu yake ya kuitwa ‘Paradiso’ imepokelewa na mashabiki tangu albamu hiyo iingie sokoni siku kadhaa nyuma.

Kupitia mahojiano na kipindi cha XXL, Stamina amesema kwamba albamu yake imepokelewa vyema na mashabiki na kwamba kila kitu ambacho yeye na timu yake walikuwa wametegemea ndicho kilichotokea.

"So far so good kila kitu kiko sawa tu tulichokitegemea ndo hicho ambacho pia kimetokea kutokana na uzito pia wa album. Sina haja ya kujisifia sana lakini watu ambao wamesikiliza album na feedback nnazopata zote yaani inaonesha kabisa album yangu ni bora kabisa. Kwa hiyo sio kwamba najisifia," alizungumza Stamina.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Stamina Adondosha Video ya Wimbo wake 'Paradiso' amshirikisha Marissa

Aidha kupitia mahojiano hayo, Stamina aliweka wazi mchango mkubwa wa marehemu Godzilla kwenye muziki wake ambapo msanii huyo ametanabaisha kuwa Godzilla aliamini katika kipaji chake hata kabla hajawa msanii mkubwa na ndo maana bado anamheshimu sana.

"Nilivyofika Dar nyimbo yangu ya kwanza kufanya ni Punch after Punch ambayo nilimshirikisha Godzilla na Izzo B. Bila maringo bila nini Zizi aliweza kufika kwa Mensen. Nilikuwa na nguo zangu za uniform kabisa na Izzo akaja palepale akanifanyia verse ilikuwa ni amani sana kwangu" aliongeza Stamina.

‘Paradiso’ ni albamu ya pili kutoka kwa Stamina tangu aanze muziki, ya kwanza ikiwa ni ‘Mlima Uluguru’ ambayo iliingia sokoni mwaka 2015 na kuweza kufanya vizuri.

Leave your comment