Izzo Bizness Aeleza Tofauti Baina ya Kiwanda cha Muziki cha sasa na Kile cha Zamani

[Picha: Mikato]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Izzo Bizness hivi karibuni amebainisha utofauti uliopo kati ya mwenendo wa muziki wa sasa na muziki wa miaka za nyuma hapa nchini Tanzania.

Akizungumza na kituo cha Times FM, Izzo Bizness ametanabaisha kuwa kwa sasa kumekuwa na mapinduzi makubwa kwenye muziki tofauti na zamani kwani studio za kurekodi ngoma zimekuwa ni nyingi.

Soma Pia: Marioo Atangaza Kuachia Albamu na EP Mpya Kwa Pamoja

Bizness pia alisema kuwa kumekuwa na maboresho makubwa kwenye vyombo vya habari ambavyo ni mhimili mkubwa wa tasnia ya muziki.

 "Kwa experience tu ambayo mimi ninayo personal kuna hatua kubwa imefanyika, mapinduzi kuanzia kwenye media houses studio zimekuwa nyingi tofauti na zamani, wasanii watu wamekuwa huru yani kuna kila aina ya muziki wafanyaji ni wapo," amezungumza Izzo Bizness.

Soma Pia: Gigy Money Atuma Ujumbe Mkali Kwa Mashabiki Wanaomkosoa Vibaya

Izzo Bizness aliongeza kwa kusema kuwa hata soko pia limebadilika kwani kwa sasa mashabiki wana uelewa mkubwa wa kupokea na kusikiliza mitindo tofauti tofauti ya muziki tofauti na aina ya mashabiki waliokuwepo miaka ya nyuma.

"Uelewa umekuwa mkubwa ukienda pia kwa mshabiki ni tofauti na zamani. Kwa sababu mimi nakumbuka kipindi narekodi ridhiwani 2011 kwa sababu nilirekodi kwenye beat ya Trap, kipindi kile beat za Trap zilikuwa zinaonekana ni ubitozi tu yaani kwamba mabeat gani haya hayana mpango," aliongeza Izzo Bizness.

Kwa sasa, Izzo Bizness anatamba na ngoma yake ya ‘Top Of The Game’ ambayo imetoka mwishoni mwa mwezi Novemba.

Leave your comment