AT Azungumzia Madai ya Uhasama Baina ya Wasanii wa Zamani na wa Kizazi Kipya

[Picha: Director AT Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mmoja kati ya wasanii wakongwe zaidi kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania AT ametoa kauli yake kuhusu mjadala wa uhusiano baina ya wasanii wa enzi ya zamani na wale wa kizazi kipya.

 Huu ni mjadala ambao umewavutia wadau mbali mbali kwenye muziki wa bongo ikiwemo rapa mwenye heshima kubwa Tanzania Professor Jay. Kwa upande wake, AT alitofautiana na dhana kwamba kuna uhasama baina ya wasanii wa kizazi kipya na waanzilishi wa muziki wa bongo.

Soma Pia: Beka Flavour Aahidi Kuachia Albamu Hivi Karibuni

Alieleza kuwa dhana hii imetokana na baadhi ya wasanii wa kizazi kipya kukataa kukosolewa pale ambapo wanaenda kombo. Alitoa mfano wake kwa kusema kuwa yeye binafsi anawaunga mkono wasanii wa kizazi kipya na anahudhuria tamasha zao.

"Nisingelikuja kwenye show ya Ibraah. Sio kweli, hizo ni dhana zimejijenga kwa sababu vijana wengine hawataki kukosolewa," AT alisema.

Soma Pia: ‘Sukari’ ya Zuchu Yaweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

Aliongezea kuwa kumeibuka fikra ya wasanii kuoneana gere na ndio maana dhana ya uhasama ikakua. Alisema kuwa wao kama wasanii wa zamani wa bongo waliwasaidia wasanii wa kizazi kipya na hivyo basi hawawezi kuwa na ubaya wowote.

"Hii mitindo ya kuonekana kwamba mtu anaonewa gere ndio inajijenga kwamba mtu fulani ana chuki, lakini sio kweli. Kwa sababu sisi sisi ndio tumesaidia na hawa hawa ambao wapo," AT aliongezea.

Leave your comment