Beka Flavour Aahidi Kuachia Albamu Hivi Karibuni

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mwenye kipaji cha kipekee kutokea nchini Tanzania Beka Flavour ameahidi kuwa yupo mbioni kuachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki.

Beka Flavour ambaye alitambulika na watanzania baada ya kujiunga na kundi la Yamoto Band aliweka wazi nia yake ya kuachia albamu kupitia mahojiano aliyoyafanya na kituo cha Times FM ambapo amefunguka na kusema kuwa yuko kwenye hatua za mwisho.

Soma Pia: Beka Flavour Akerwa na Madai ya Kufeki Ajali Kwa Sababu ya Kiki

"Mimi matamanio yangu niwe na album na nitalifanikisha hilo kwa sababu niko kwenye hatua za mwisho unajua watu wajue kuwa albamu sio kitu rahisi lakini kila kitu kiko sawa lakini mwishoni itatoka. Watu waendelee kunisapoti," alizungumza mkali huyo wa ngoma ya ‘Sikinai’.

Kauli hii kutoka kwa Beka Flavour inakuja takriban miezi mitatu tangu msanii huyo atetemeshe kiwanda cha muziki nchini Tanzania kwa kuachia ngoma yake ya ‘Kama Siwezi’ ambayo imeweza kufanya vizuri hapa nchini.

Soma Pia: Beka Flavour Afichua Sababu Kuu Iliyofanya Yamoto Band Kuvunjika

Kama Beka Flavour ataachia albamu hii kama alivyopanga, basi atakuwa ni msanii wa pili kutokea kundi la Yamoto Band kuachia albamu baada ya Mbosso ambaye mwanzoni mwa mwaka huu aliachia albamu yake yenye hadhi ya nyota ya tano ya kuitwa ‘Definition Of Love’.

Kwingineko , wasanii wengine ambao wako mbioni kuachia albamu ni pamoja na Diamond Platnumz, Rosa Ree, Marioo, Nay wa Mitego na wengine wengi.

Leave your comment