Beka Flavour Akerwa na Madai ya Kufeki Ajali Kwa Sababu ya Kiki

[Picha:Beka Flavour Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki wa bongo Beka Flavour ameelezea kukerwa na baadhi ya ripoti zinazodai kuwa alifeki ajali ili kutafuta kiki ya kujiongezea umaarufu kwenye muziki.

Ripoti hizi ziliiibuka muda mfupi baada ya msanii huyo kuwafahamisha mashabiki wake kuwa alikumbwa na ajali ya barabara ila kwa bahati nzuri alinusuruka bila majeraha.

Soma Pia: Rais Samia Awafurahisha Watanzania Baada ya Kutaja Marioo, Harmonize Kwenye Hotuba Yake

Beka Flavour aliambatanisha ujumbe huo na baadhi ya picha ambazo zilipigwa kwenye eneo la ajali.

Muda sio mrefu baada ya kuchapisha ujumbe huo, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walidai kuwa huenda msanii huyo alikuwa anatafuta kiki ili kuijiiongeza umaarufu kwenye tasnia ya muziki.

Soma Pia: Rayvanny Adokeza Ujio wa Kolabo Baina Yake na Justin Bieber

Madai haya yanatokana na kuongezeka kwa visa vya wasanii wa bongo kutafuta kiki. Beka Flavour kupitia ukurasa wake wa Instagram alikanusha madai hayo na kuonyeshwa kukerwa na jinsi watu walikosa kuamini kuwa yaliyomkumba yalikuwa ya kweli.

Alisema kuwa sio jambo la kufarahisha wakati kila jambo analofanya msanii linatafsiriwa kuwa njia ya kutafuta kiki.

Beka Flavour alijitetea na kusema kuwa alichapisha picha hizo za ajali pamoja na ujumbe, si kwa sababu ya kutaka usaidizi, bali kwa sababu ya kuwafahamisha mashabiki wake kile ambacho alikuwa amepitia.

"Kumradhi, naposti hii kitu sio kama napenda, no!. Ni katika kuwaaminisha tu, wale ambao waliamini kuwa hii kitu ni kiki jamani Watanzania tulipofikia ni pabaya tena sana yaani kila mmoja wetu huko alipo ameshaaminishwa kuwa kila kitu kimtokeacho mtu anayeitwa msanii basi ni kiki. Dah!" Kipande cha ujumbe wa Beka Flavour kilisomeka.

Leave your comment