Chidi Benz Adai Mgwanyiko wa Wasanii Unaathiri Vibaya Tasnia ya Muziki Tanzania
1 December 2021
[Picha: GetMziki]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mmoja kati ya marapa wakongwe zaidi kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania Chidi Benz amefunguka kuhusu jinsi mgawanyiko wa wasanii unaathiri vibaya muziki wa bongo.
Chidi Benz akizungumza wakati wa kutambulisha albamu yake mpya ambayo imepewa jina la 'Wa2Wangu', alisema kuwa uhasimu na mgawanyiko uliopo baina ya makundi tofauti ya wasanii nchini Tanzania una athari kubwa katika ukuaji wa tasnia ya muziki nchini humo.
Soma Pia: Diamond, Rayvannny, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Novemba
Alieleza kuwa wasanii wamejitenga katika makundi tofauti na kujiundia mazingira ya kujikuza wao wenyewe, huku wasanii wengine wakiachwa kujipigania.
Chidi Benz alitoa mfano jinsi wasanii wa Hip-hop nchini Tanzania walikosa uteuzi katika tuzo za AFRIMA, kwa sababu ya mgawanyiko huo. Kwa mujibu wa Chidi Benz, mgawanyiko huo umeathiri hadi sekta zingine za tasnia ya muziki na burudani ikiwemo uanahabari.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Dulla Makabila Aachia Ngoma Mpya ‘Nipe Mkono Tushindane’
Rapa huyo alisema kuwa si jambo nzuri wasanii kugawanyika, alisisitiza kuwa kunafaa kuwepo na umoja baina ya wasanii wa bongo.
"Muziki sasa hivi umekuwa wakina fulani familia yao hii hapa, wana redio yao, wana tv yao, wana ofisi yao, wana michongo yao, wana vitu vyao. Kama wanapata namba ya kwenda sijui huko Afrima wanapeana wao. Ina maana wao kama hawawezangi, hawajui sio wakali, wao wanapata tabu kuenda ama wakienda hawapati pia. Kwa hivyo inaonekana Hip Hop sasa hivi ahapajachaguliwa mtu," Chidi Benz alisema.
Leave your comment