Nyimbo Mpya: Dulla Makabila Aachia Ngoma Mpya ‘Nipe Mkono Tushindane’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Gwiji wa muziki wa singeli Dulla Makabila ameachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la ‘Nipe Mkono Tushindane’.

Kwenye ngoma hii yenye mahadhi ya singeli, Dulla Makabila anatoa changamoto kwa wapinzani wake akiwaambia kuwa hawamzidi kwa chochote iwe kipesa au kiserikali.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Ibraah, Nandy na Maua Sama Tanzania Wiki Hii 

"Nikimpa mtu heshima yangu asiponirudishia nachukua kwa nguvu. Kwanza hauniwezi kiserikali, hauniwezi kwa hela hauniwezi kwa mademu, hauniwezi kwa uchawi. Na kama unabisha nimpe mkono tushindane," anaimba Dulla Makabila kwenye aya ya kwanza ya ngoma hii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Stamina Aachia Albamu Yake ‘Paradiso’

Mashahiri ya ngoma hii hasa kwenye aya ya kwanza yameonekana kushabihiana sana na kauli ambayo aliitoa Harmonize kwa waandishi wa habari hivi karibuni.

Akizungumza na wanahabari, Harmonize alisema kuwa kipindi alikuwa kwenye lebo ya WCB, Diamond Platnumz aliwahi kumwambia kuwa hamuwezi kipesa wala kiserikali, na kama anabisha Harmonize atoe mkono ili ashindane na Diamond Platnumz.

Watu wengi wameguswa na wimbo huu kutokana na ufundi wa Dulla Makabila kuweza kuchukua kauli ya Harmonize na kuifanya kuwa wimbo na pia namna ambavyo Dulla Makabila ameweka vionjo tofauti tofauti vya kuchangamsha mashabiki.

Kabla ya ngoma hii, Dulla Makabila alikuwa anatamba na ngoma yake ya ‘Ukizipata’a ambayo iliingia sokoni takribani wiki mbili zilizopita.

https://www.youtube.com/watch?v=M7T-ExLY64g

Leave your comment