Nyimbo Mpya: Stamina Aachia Albamu Yake ‘Paradiso’

[Picha: East African TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Stamina ameachia albamu yake mpya yenye jina la ‘Paradiso’.

Albamu ya ‘Paradiso’ imesheheni nyimbo 13 za moto na kati ya hizo ni moja tu ambayo ameimba peke yake nyingine zote ameshirikiana na wasanii tofauti tofauti kama Kayumba, Saraphina, Aslay, Isha Mashauzi, Barakah The Prince na wasanii wengine wengi.

Soma Pia: Rayvanny Aingia Kwenye Chati za Billboard Latin

Aidha, Stamina ameshirikiana na watayarishaji tofauti tofauti wa muziki katika kuaandaa albamu ikiwa ni pamoja na Bear, Sampamba, Papa Shaska na Walter Chilambo ambaye pia ni mwanamuziki kutoka Tanzania.

Wakati anatambulisha albamu hii kupitia ukurasa wake wa Instagram, Stamina aliwashukuru wote walioshiriki katika maandalizi ya albamu yake kwa kuandika "Shukrani zangu za dhati ziende kwa wasanii wote ambao nimeshirikiana nao kwenye hii album, producers wote, directors wote na wadau wote tuliopambana kukamilisha albamu hii."

Soma Pia: Beka Flavour Akerwa na Madai ya Kufeki Ajali Kwa Sababu ya Kiki

Kutokana na albamu hii, Stamina anaingia kwenye orodha ya wasanii wa Hip-hop ambao wameachia albamu kwa mwaka huu. Wengineo ni pamoja na Dogo Janja na albamu yake ya ‘Asante Mama’ pamoja na Rapcha na albamu yake ya ‘Wanangu 99’.

Leave your comment

Top stories