Rayvanny Aingia Kwenye Chati za Billboard Latin

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Rayvanny ameweka rekodi mpya kwenye muziki wake baada ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kuonekana kwenye chati za muziki za Billboard Latin za huko Amerika ya kusini.

Rayvanny ameweka rekodi hiyo kupitia ngoma ya ‘Mama Tetema’ ambayo ameshirikiana na mwanamuziki Maluma kutokeo Columbia.

Soma Pia: Rayvanny Adokeza Ujio wa Kolabo Baina Yake na Justin Bieber

Ngoma hiyo ya ‘Mama Tetema’ iliyoachiwa wiki mbili zilizopita imefika namba 12. Hata hivyo Rayvanny sio mgeni kwenye chati za Billboard kwani ngoma ya ‘Jollof On The Jet’ aliyoshirikishwa na DJ Cuppy kutokea Nigeria mwishoni mwaka jana iliingia kwenye chati za muziki za Top Triller Global.

Ngoma ya ‘Mama Tetema’ ni ngoma ambayo imefungua fursa nyingi za kimuziki kwa Rayvanny kwani kupitia ngoma hiyo Rayvanny aliweza kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA ambazo zilifanyika huko nchini Hungary Novemba 14 mwaka huu.

Soma Pia: Anjella Atangaza Ujio wa EP Yake ya Kwanza Tangu Aanze Muziki

‘Mama Tetema’ ni ngoma ambayo imetokana na ngoma ya ‘Tetema’ iliyotoka mwaka 2019 ambayo Rayvanny alimshirikisha Diamond Platnumz.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Maluma alionekana kupitia akaunti yake ya Instagram akicheza wimbo huo na baada ya Rayvanny kuweka kipande cha video hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram, Maluma aliweka maoni kwenye video hiyo kwa kuandika ‘Remix’; kitu ambacho kwa wengi kiliashiria kuwa tetema remix iko jikoni.

Kwa sasa video ya ngoma hiyo imeshatazamwa takribani mara Milioni 7.9 kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment