Anjella Atangaza Ujio wa EP Yake ya Kwanza Tangu Aanze Muziki

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa kizazi kipya Anjella ametangaza ujio wa EP yake ya kwanza tangu aanze taaluma yake ya muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye 'Insta Stories', Anjella aliweka wazi tarehe kamili ambayo ataachia EP hiyo.

Tarehe tano, mwezi Disemba mwaka huu ndio itakuwa siku rasmi ambayo EP hiyo itatoka.

Soma Pia: Wasifu wa Anjella, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mafanikio, Mahusiano na Thamani Yake

Anjella, hata hivyo, hakufichua idadi ya nyimbo ambazo ziko kwenye EP hiyo. Msanii huyo hakutoa maelezo mengi ambayo yangechora picha ya jinsi EP yake itafanana haswaa wale waliohusika kuitengeneza ikiwemo kolabo na watayarishaji wa muziki.

Mashabiki wa Black Angel, kama jinsi anvyojiita kiutani, wako na hamu kubwa sana kwani hii ndio itakuwa EP yake ya kwanza tangia aingie kwenye tasnia ya muziki takriban miezi minane iliyo pita.

Anjella, vile vile, anasubiriwa kuwa kwenye albamu ya DJ Neptune kutoka Nigeria. Kwenye albamu hiyo Anjella ameshirikiana na bosi wake Harmonize kwenye wimbo uliopewa jina la 'My Woman'.

Soma Pia: Anjella Afunguka Kushindanishwa na Zuchu, Nandy

Anjella alitambulishwa rasmi kama mwanachama wa lebo ya Konde Music Worldwide mnamo tarehe 11 mwezi Machi mwaka jana.

Akiwa na umri wa miezi minane ndani ya Konde Music, tayari ashatoa jumla ya nyimbo nne ambazo ni pamoja na ‘Kama’, ‘Nobody’, ‘Nobody Remix’ na ‘Sina Bahati’.

Anjella kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wa kike kutoka Tanzania ambao wanasikizwa mno na apia wenye ushawishi mkubwa kwenye muziki.

Leave your comment