Anjella Afunguka Kushindanishwa na Zuchu, Nandy

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii mashuhuri kutoka Konde Music Worldwide Anjella hivi karibuni ametoa kauli yake kuhusu kushindanishwa na wanamuziki wenzake wa kike wakiwemo Nandy na Zuchu.

Ni nadra sana kumsikia Anjella akiwazungumzia wasanii wenzake haswaa wale ambao anakisiwa kuwa na ugomvi. Hivyo basi kauli hii aliyoitoa akizungumza na wanahabari ilikuwa ya kipekee.

Soma Pia: Ibraah Amsifu Anjella, Amtaja Msanii wa Kike Mwenye Bidii

Anjella alidai kuwa yeye huwa hafuatilii wanamuziki anaoshindanishwa nao. Msanii huyo hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu uhusiano wake na washindani wake.

Kauli yake Anjella iliibua gumzo mitandaoni haswaa ikizingatiwa kuwa siku chache zilizopita msanii mwenzake Zuchu alijipata katika hali sawia ambapo aliulizwa kutoa kauli kuhusu Nandy.

Soma Pia: Anjella Ampongeza Country Wizzy Kwa Mafanikio Yake Kimuziki

Tofauti na Anjella, Zuchu almsifia Nandy kama msanii mwenye bidii ambaye anafanya vizuri sana. Japo Anjella hana tofauti za kibafsi na Zuchu, ushindani wao unatokana na uongozi wa lebo walikosainiwa.

Anjella amesainiwa katika lebo ya Konde Music Wordwide inayosimamiwa na Harmonize. Zuchu kwa upande mwingine amesainiwa katika lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Diamond Platnumz na Harmonize walikua marafiki wa karibu kabla ya tofauti kuibuka baina yao na kuwafanya mahasimu. Nandy kwa upande mwingine ni rafiki wa karibu wa msanii Alikiba ambaye ni mshindani mkubwa wa Diamond.

Licha ya haya yote, wasanii hawa wa kike hawajahi kukosana au kujibizana mitandaoni. Zuchu, Nandy na Anjella ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaopeperusha bendera ya Tanzania katika sekta ya muziki na wote wanafanya vizuri sana.

Leave your comment