Anjella Ampongeza Country Wizzy Kwa Mafanikio Yake Kimuziki

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi Anjella kutokea Konde Music Worldwide amejitokeza na kumpongeza mwenzake kutokea lebo hiyo hiyo Country Wizzy kwa hatua alizopiga kimuziki.

Katika chapisho ambalo Anjella aliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, alimsifia Country Wizzy kama msanii mwenye bidii na wa kujituma. Kulingana na Anjella muziki umekua kitambulisho cha Country Wizzy kwa muda mrefu.

Soma Pia: Ibraah Amsifu Anjella, Amtaja Msanii wa Kike Mwenye Bidii

Aliongeza kuwa Country Wizzy amekua mfano wa kuiga miongoni mwa vijana haswaa wasanii wanaochipuka.

Anjella alisistiza kuwa Country Wizzy amefanya kazi nzuri katika kukuza muziki wa kizazi kipya. Aliwahimiza wafuasi wake kumuunga mkono Country Wizzy katika taaluma yake ya muziki.

Soma Pia: Anjella Ashukuru Konde Music Worldwide Kwa Kumkuza Kimuziki

"Muziki umeendelea kuwa kitambulisho kikubwa kwenye career yake, inspiration kubwa kwa vijana wapya wanaochipukia kwenye game ni miongoni mwa nguzo zake," Anjella alisema katika chapisho lake mtandaoni.

"Pongezi kwa The Father Of New Generation @countrywizzy_tz kutokana na mengi anayofanya kwenye game na kuendelea kuwakilisha kizazi KIPYA na muziki mzuri," aliongezea kwenye chapisho hilo.

Country Wizzy alimshukuru Anjella kwa ujumbe wake kwenye sehemu ya maoni ya chapisho hilo.

Anjella pia amesifiwa kwa juhudi zake za muziki. Ni mmoja wa wasanii wa kike nchini Tanzania wenye ushawishi mkubwa na wafuasi wengi. Amepanda ngazi na kuwa mmoja wa wasanii wanaoheshimika Afrika Mashariki.

 Kufikia sasa nyimbo za Anjella zimepokelewa vyema na mashabiki na kutazamwa mara mingi sana. Nyimbo zake zimefikia kiwango cha kupata mamilioni ya watazamaji.

 

Leave your comment